SUALA la kujitambua na kutambua nini mahitaji yako ni moja ya chanzo cha mabadiliko yanayohitajika katika maisha, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Joyce Msuya amebainisha.
Alisema hayo akizungumza na wanawake mbalimbali waliofika kusikiliza historia yake na jinsi alivyoweza kumudu maisha ya mama, mke na mfanyakazi katika mashirika mbalimbali ya kimataifa na kupanda ngazi.
Aidha alisema pamoja na kujitambua mtu anatakiwa kufanya kazi kwa kuwajibika, kujisukuma zaidi katika kazi na kufanya maamuzi ya kushirikisha familia hasa patna.
Msuya ambaye alianza kazi ya UNEP mwaka huu mwezi wa nane baada ya kupitia Benki ya dunia na mashirika mengine kadhaa alisema mfumo wa Tanzania wa shule, malezi ndiyo iliyofanya kuunganisha nguvu, uwezo na ujasiri wa kuweza kufanya mambo ambayo yamemfanya kupata nafasi kubwa zaidi.
Alisema mfumo wa Tanzania wa maisha umekuwa msukukumo mkubwa kwake kwani aliweza kuishi na watu tofauti na kuvumilia huku akitekeleza wajibu wake kwa kujiongeza zaidi.Alisema kutokana na juhuzi za wazazi wake katika kusimamia malezi aliweza kupata maarifa zaidi ya kuishi kwa kuhudhuria shule za umma za Forodhani, Jangwani na Weruweru kisha kuchukua mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) Mafinga na kumalizia mafunzo hayo Mlalakua.
“Ukweli ni kuwa wazazi wangu walitaka tuishi maisha ya kawaida kama watanzania wengine ndiyo maana walinipeleka shule za bweni na kuhakikisha naenda jeshini. “ alisema Mkurugenzi huyo ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Anasema malezi ya kujitegemea yamemfanya awe na uwezo wa kufanya bajeti hali ambayo ilimwezesha kuishi vyema Scotland na hata alipoenda kuchukua shahada yake ya pili nchini Canada.“Kusema ukweli Baba na mama walinitengenezea mfumo mzuri wa kuishi hasa pale walipojenga na kunihimiza kufanya kazi na kusoma wakati nikiwa mdogo.” Alisema Msuya.
Anasema amevuka vigingi vingi hasa kwenye muwashawasha wa masomo lakini kama walivyo watu wote alifanya maamuzi makini kuzingatia ushauri na kile anachokipenda.
Akiulizwa nini hasa kinamsukuma, alisema kwamba familia ni kitu muhimu kwake na kwamba amefanya mambo mengi akiwa na familia yake kuanzia mume wake ambaye wamo katika ndoa kwa miaka 20 na kujaliwa kuwa na watoto wawili.
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP,
Bi. Joyce Msuya akizungumza viongozi wanawake vijana kwenye mdahalo
ambapo aliutumia kuhamasisha wanawake wengine kujituma uliofanyika
mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Bi. Natalie Boucly.
Mkurugenzi
wa uendeshaji wa Doctors’ Plaza, Bi. Sophia Byanaku akiuliza swali kwa
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) wakati wa mdahalo
maalum kwa viongozi wanawake vijana ambapo walipata fursa ya
kuhamasishwa kujituma na kujitambua uliofanyika mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya viongozi wanawake vijana walioshiriki kwenye mdahalo ulioendeshwa na
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) ambapo aliutumia
kuhamasisha wanawake wengine kujituma uliofanyika mwishoni mwa wiki
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es
Salaam
Baadhi
ya viongozi wanawake vijana wakiuliza maswali kwa Naibu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce
Msuya (hayupo pichani) wakati wa mdahalo maalum uliotumika kuhamasisha
wanawake wengine kujituma na kujitambua ambapo umefanyika mwishoni mwa
wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar
es Salaam
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP,
Bi. Joyce Msuya katika picha ya pamoja na viongozi wanawake vijana mara
baada ya kumalizika kwa mdahalo huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...