Mwenyekiti wa Kamati ya  Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Hans Poppe leo Oktoba 16, 2018 ameunganishwa katika kesi ya kughushi nyaraka za klabu na utakatishaji wa fedha inayomkabili Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu,
Baada ya kuunganishwa katika kesi hiyo, wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro amewasomea washtakiwa wote  mashtaka 10 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.  Katika mashitaka hayo 10, Hanspope anakabiriwa na mashtaka 2,  shtaka moja ni la kuwasilisha nyaraka za uongo na shtaka lingine ni la kughushi.
Katika mashtaka hayo 10, yamo ya kula njama, kutoa nyaraka za uongo, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi, utakatishaji fedha, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kuendesha biashara bila kufuata sheria. Katika shitaka la utakatishaji Aveva na Kaburu wanahusishwa na shtaka la kutakatisha kiasi cha dola 300,000 (zaidi ya sh. Milioni 650).


Katika shitaka la kughushi linalowakabili washtakiwa wote, imedaiwa Machi 15, 2016 washtakiwa kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577, zaidi ya Sh. Milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.
Pia katika shtaka jingine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya March 10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

Hata hivyo, shtaka la mwisho halikusomwa kwa sababu linamuhusu mshtakiwa 4  Franklin  Lauwo ambaye bado hajafikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewa mashtaka yao Mahakama ilitoa masharti ya dhamana kwa Hans Poppe yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.milioni 15 kila mmoja, 
Mshtakiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huku Aveva na Kaburu wakirudishwa rumande kwa kuwa mashtaka dhidi yao hayana dhamana.  Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 19, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya  Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hanspope akiwa na  Makamu Rais wa Simba SC Godfrey Nyange "Kaburu"  katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam leo Oktoba 16, 2018
Mwenyekiti wa Kamati ya  Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hanspope (kushoto) akiwa na Rais wa klabu ya Simba  Evans Aveva (kulia) na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...