Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi Kituo chá Polisi kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya sh.milioni 75  ili kiweze kutoa huduma kwa jamii  inayozunguka eneo la Changanyikeni Kibada jijini Dar es Salaam.

Ujenzi wa kituo hicho kwa NHC sera ya utekelezaji wa huduma kwa jamii  katika sehemu mbalimbali zilizokuwa  na miradi  na hata sehemu zingine ambapo miradi haifayiki.. 

Akizungumza kabla ya ufunguzi na makabidhiano, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi amesema kuwa  kabla ya ujenzi wa nyumba 248  za shirika hilo katika eneo la Kibada, walipanga kujenga kituo hicho ambacho sasa  kimesha kamilika ikiwa kuhakikisha wakazi wanaoishi katika nyumba hizo wanakuwa na ulinzi wao na mali zao.

Amesema kituo hicho chenye vyumba viwili vya mahabusu (wakiume na wakike), ofisi ya mkuu wa kituo, vyoo viwili vya maofisa na vya mahabusu.

"Kumekuwa na mawasiliano na  Jeshi la Polisi kukifanyika kwa  maboresho kabla ya kukikabidhi kwa kuhakikisha  kituo kimekidhi viwango vya ubora vya  mahitaji ya polisi na kitawahudumia wakazi wengi wa eneo hili, "amesema Maagi.

Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadhi Haji, alilishukuru shirika hilo kwa kuonesha uzalendo na kueleza kuwa, usalama ni muhimu  kwa wananchi ili waweze kuishi kwa amani na kujiletea maendeleo.
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadhi Haji akizungumza katika halfa ya makabidhiano ya kituo cha polisi Kibada kilichojengwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi akizungumza kuhusiana na ujenzi wa kituo cha polisi ikiwa ni sera ya shirika hilo katika hafla makadhibiano ya kituo polisi yaliyofanyika Kibada jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Changanyikeni, Gwalugano Mwakatobe akieleza umuhimu wa kujengwa kwa kituo cha polisi katika eneo lake katika hafla ya makabidhiano ya kituo cha polisiliyofanyika kibada jijini Dar es Salaam.
 .Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadh Haji akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha Polisi 
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadh Haji akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Kibada na . Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi
Muonekano wa Kituo cha Polisi cha NHC Changanyikeni 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...