Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi Kituo chá Polisi kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam klichojengwa kwa thamani ya zaidi ya 
sh.milioni 75 ili kiweze kutoa huduma kwa jamii inayozunguka eneo la Changanyikeni Kibada jijini Dar es Salaam.Ujenzi wa kituo hicho kwa NHC sera ya utekelezaji wa huduma kwa jamii katika sehemu mbalimbali zilizokuwa na miradi na hata sehemu zingine ambapo miradi haifayiki.. 

Akizungumza kabla ya ufunguzi na makabidhiano, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi, amesema kuwa kabla ya ujenzi wa nyumba 248 za shirika hilo katika eneo la Kibada, walipanga kujenga kituo hicho ambacho sasa kimesha kamilika ikiwa kuhakikisha wakazi wanaoishi katika nyumba hizo wanakuwa na ulinzi wao na mali zao.

Amesema kituo hicho chenye vyumba viwili vya mahabusu (wakiume na wakike), ofisi ya mkuu wa kituo, vyoo viwili vya maofisa na vya mahabusu.
"Kumekuwa na mawasiliano na Jeshi la Polisi kukifanyika kwa maboresho kabla ya kukikabidhi kwa kuhakikisha kituo kimekidhi viwango vya ubora vya mahitaji ya polisi na kitawahudumia wakazi wengi wa eneo hili, "amesema Maagi.

Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji, alilishukuru shirika hilo kwa kuonesha uzalendo na kueleza kuwa, usalama ni muhimu kwa wananchi ili waweze kuishi kwa amani na kujiletea maendeleo."Sasa ni jukumu letu kukitunza kituo hiki na kuwalinda wananchi na mali zao. Hata hivyo kwa asilimia mia moja hatutaweza peke yetu bila wananchi kushirikiana nasi kufichua uhalifu na wahalifu, "alisema Kaimu Kamanda Haji. 

Haji ambaye pia alimwakilisha Kamanda wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa, amesema kituo hicho kwa sasa kitatoa huduma kwa saa 12 kutokana na kuwa ni kidogo na NHC wamekubali kukiongeza ili kiongeze huduma kwa kufanya masaa 24 na kuhimiza kuunda kikundi cha ulinzi shirikishi ili kushifikiana na polisi kuimarisha ulinzi zaidi. 

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Changanyikeni, Gwalugano Mwakatobe, aliishukuru NHC na kuekeza kuwa, awali walilazimika kutembea zaidi ya kilometa tisa kufuata huduma na uwepo wa kituo hicho utaimarisha usalama na kuondoa ubambikizaji wa kesi kwa raia.

Aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo hicho, Jacob Daqaro, aliwaomba wananchi ushirikiano na kuahidi kusimamia sheria, haki na usalama. Kituo hicho kipo katika eneo lá mradi wa nyumba 208 za NHC Kibada, Kigamboni na Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Nyumba hizo, Juvenil Mwambi, alishukuru Polisi kwa kuanza kazi jana mara baada ya makabidiano na kusisitiza ushirikiano.
 .Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadh Haji akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha Polisi 
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadh Haji akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Kibada na . Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi
Muonekano wa Kituo cha Polisi cha NHC Changanyikeni .

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadhi Haji akizungumza katika halfa ya makabidhiano ya kituo cha polisi Kibada kilichojengwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi akizungumza kuhusiana na ujenzi wa kituo cha polisi ikiwa ni sera ya shirika hilo katika hafla makadhibiano ya kituo polisi yaliyofanyika Kibada jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Changanyikeni, Gwalugano Mwakatobe akieleza umuhimu wa kujengwa kwa kituo cha polisi katika eneo lake katika hafla ya makabidhiano ya kituo cha polisiliyofanyika kibada jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...