Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo zilizotolewa na NMB ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

BENKI ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 na kushirikisha wachezaji wa gofu kutoka klabu mbalimbali nchini.

Udhamini uliotolewa ni wa shilingi milioni 26 pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo jezi zitakazo tumika katika mashindano hayo vimekabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga katika viwanja vya Lugalo.Kukabidhiwa kwa udhamini huo ni mwendelezo wa Benki ya NMB kudhamini na kusaidia shughuli anuai za michezo hususani ya Jeshi la wananchi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kukabidhiwa kwa udhamini huo, Makamu Rais wa Umoja wa Klabu za Golf Tanzania, Luteni Canali David Luoga alisema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali vya golf Tanzania na makundi ya wachezaji wakiwemo watoto.Alisema mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa siku moja pekee na kufunguliwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo washindi watajipatia fedha taslimu pamoja na vikombe.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yatakuwa na mvuto wa pekee kwa kile kushirikisha viongozi waandamizi mbalimbali kutoka Serikalini waliostaafu na awaliopo madarakani."Kama unavyofahamu klabu yetu ya mchezo wa golf inashirikisha pia viongozi mbalimbali waandamizi kutoka Serikalini waliostaafu na wengine bado wapo madarakani nao tunatarajia watashiriki katika mashindano haya...hivyo yatakuwa na mvuto wa kipekee," alisema Luteni Canali Luoga.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 26 Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo (katikati) zilizotolewa na NMB kudhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...