Timu ya Uchunguzi ya wasindikizaji wa Kahawa ya magendo yaundwa
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Nchini limetuma kikosi cha uchunguzi kufatilia tuhuma za askari waliokuwa wakisindika Kahawa ya Magendo wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Uchunguzi huo unatokana na kauli ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ya kutaka kufanyika uchunguzi kwa askari hao waliohusika kusindikiza Kahawa ya magendo.

Akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es Salaam Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa amesema katika uchunguzi huo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kyerwa (OCD) Justine Joseph ameshushwa cheo pamoja na kuhamishwa katika Kituo cha kazi.

Amesema aliyekuwa OCD wa Wilaya Kyerwa Justine Joseph amehamishiwa mkoani Iringa na kuwa chini ya uangalizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa.

Amesema uchunguzi huo ukikamilika watatoa  majibu kwa wale  waliohusika na tuhuma za usindikizaji wa Kahawa ya magendo.

Aidha amesema kuwa wakati Polisi  wanafanya operesheni wananchi wanatakiwa kutii amri hiyo.

Mwakalukwa amesema tukio lilotokea mkoani Songwe la Mtu kupigwa risasi ilitokana na wananchi kutotii amri ya polisi wakati wakifanya operesheni ya waganga wa jadi lambalamba.

"Amri ya Polisi inatakiwa wananchi watii ili kuweza kuepuka na madhara yatayotokea mara baada ya kusaidia"amesema Mwakalukwa.Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...