Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji nchini kote kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba, kwani kufanya hivyo kunawaondolea fursa ya kuendelea na masomo pindi wanapofaulu.

Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Hakikisheni watoto wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwani wanapofika huko wanarubuniwa na waajiri hivyo hata matokeo yakitoka na kuonesha kuwa wamefaulu hawarejei kuendelea na masomo “alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.

Kiongozi huyo ameendelea kuwasisitiza wazazi kuwa fursa za Elimu katika nchi yetu ni kubwa, ikizingatiwa kuwa Elimu msingi ni bure hivyo hakuna kisingizio tena kuwa mtoto hawezi kusoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipokelewa na Watendaji wa Mkoa wa Manyara wakati alipowasili mkoani hapo kwa ajili ya kupata taarifa ya Elimu ya Mkoa huo. Naibu waziri huyo yuko Mkoani Manyara kwa ziara ya siku tatu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na kuangalia hali ya Elimu katika mkoa husika.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa maelekezo kwa Viongozi na watendaji wa VETA Manyara wakati wa kukagua karakana inayotumika na wanafunzi wanaosoma kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro Mechanics).

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa karakana itakayotumiwa na wanafunzi wanaosoma kozi ya ufundi uwashi katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Manyara. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...