Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema kuwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni chombo muhimu katika kuzalisha mafundi watakaohudumia viwanda vinavyojengwa nchini.

Ole Nasha ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni kujua utendaji wa mamlaka hiyo katika uzalishaji wa ujunzi kwa vijana nchini, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipambanua kuwa ni nchi viwanda hivyo licha ya kuwepo kwa wahandisi ni lazima kuwepo kwa mafundi.

Amesema kuwa VETA ni lazima waonyeshe njia katika uzalishaji wa vijana wenye ujuzi ambao watatumika katika viwanda na miradi mbalimbali ya serikali inayojenga wakiwemo mafundi wa reli.

“Wahandisi kazi yao kuweka michoro lakini kazi ya kujenga ni mafundi hivyo ni wajibu wenu VETA wa kuzalisha rasimali hiyo katika ujenzi wa taifa na kazi yenu inaonekana baadhi ya vijana wamemaliza shahada ya kwanza na sasa wanajiunga mafunzo ya ufundi stadi”.amesema Ole Nasha.

Ole Nasha amesema kuwa vyuo vyote vinatakiwa kuangaliwa mitaala na VETA na visivyo na vigezo wavifungie

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya VETA , Peter Maduki amesema kuwa wanajenzi wa vyuo vya VETA kata Mikoa Mitatu na Wilaya moja moja ambavyo vitagharimu sh. bilioni 38.

Amesema Mikoa vitavyojengwa vyuo vya ufundi Geita , Simiyu , Rukwa pamoja wilaya ya Chato ikiwa kuhakikisha kila mkoa unakuwa na chuo cha ufundi stadi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk.Pancras Bujulu amesema kuwa changamoto yake ni kutafuta fedha kwa ajili ya kuismamamisha Vete.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na Menjejimenti ya VETA pamoja na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi na Menejimenti katika Mkutano na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...