Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametoa shilingi Milioni 50 kwa timu ya Taifa ya Tanzania. Fedha hizo ni kwa ajili ya safari ya mchezo wa marudiano baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Lesotho utakaochezwa Novemba 16, mwaka huu. 
 Akiwa anazungumza na wachezaji na viongozi katika hafla ya chakula cha Mchana Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt Magufuli amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya safari na sio kwa wasindikizaji. 
 “Nawapa Millioni 50 kwa ajili ya safari ya Lesotho, fedha hizi zitumike kwa ajili ya wanaotakiwa kusafiri tu, sio mambo ya wachezaji 15, viongozi wasindikazaji 30. Haya mambo yafikie mwisho.” amesema Dkt Magufuli. Mbali na hilo amewataka wachezaji kujituma na kuacha mambo ya kihuni, "Wachezaji wasipoacha uhuni watakuwa wanafunga magoli mengine ila ya uwanjani watashindwa" Taifa Stars katika mchezo uliopita dhidi ya Cape Verde walifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-0 mechi iliyopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa na kufikisha jumla ya alama 5 akishika nafasi ya pili nyuma ya Uganda.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ambao walifika Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Miguu la Tanzania TFF, BMT pamoja na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya Taifa kutoka kwa Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni mara baada ya kumkabidhi Jezi ya Timu ya Taifa.
 Beki wa Timu ya Taifa Shomari Kapombe akijitambulisha mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakabidhi Shilingi milioni 50, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi wa TFF ili zitumuke katika maandalizi ya mechi inayokuja ya kuwania kufuzi AFCON nchini Cameroon. Wengine katika picha ni Rais wa TFF Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo mara baada ya kukabidhi Shilingi milioni 50 kwa TFF kwa ajili ya Maandalizi ya  Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam. P
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Taifa Stars mara baada ya kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha mstari wa Mbele ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe watatu kutoka kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga watatu kutoka kulia akifatiwa na Leodgar Tenga Mwenyekiti wa BMT, kocha wa timu ya Taifa Emanuel Amunike Pamoja na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao. Wengine ni Rais wa TFF Wallace Karia akiwa pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kipa wa Timu ya Taifa Aishi Manula mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Beki kisiki wa Taifa ya Tanzania Kelvin Yondani mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...