Na Vero Ignatus, Karatu


MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Wilaya ya Karatu, Edward Mwakapaju kuhakikisha mtumishi wa shirika hilo aliyechukua pesa kiasi cha Sh. 70,000/= kwa mmoja kati ya mwananchi wa eneo la Mang'ola badala ya Sh. 27,000/= za kuunganishiwa umeme wa REA kuzirudisha mara moja.

Gambo  amesema kuwa haridhishwi na kasi ya usambazwaji umeme unaofanywa na Kampuni ya NIPO Group Ltd kwenye vijiji na vitongoji mbalimbali vya wilaya hiyo na kumpa agizo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Henry Mhina kuhakikisha anachukua hatua ili wananchi waweza kuunganishiwa umeme.

RC Gambo  aliyasema hayo katika ziara yake ya siku tatu kwaajili ya kukagua miradi ya umeme wa Vijijini ( REA) miradi ya maji  na barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

Alisema mtumishi huyo wa Tanesco (jina hakumtaja) alichukua fedha kwa mwananchi wa Man'gola kiasi cha Sh. 70,000 ili amuunganishie umeme wa REA ilihali akijua kuwa gharama ya kuunganisha umeme huo ni Sh. 27,000/= huku wananchi wengine wa vijiji vya Tloma na Ganako wakitozwa Sh. 177,000/= badala ya Sh. 27,000/=.  

Alisema ingawa mtumishi huyo wa Tanesco amefukuzwa kazi lakini hela alizochukua Sh. 70,000/= kutoka kwa mwananchi huyo haijarudishwa hivyo ni vyema sasa hela hizo zikarudishwa kwa mwananchi huyo mara moja huku akiziagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia tatizo hilo mara moja.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo wakipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa TARURA wilaya ya Karatu juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Getamong wilayani humo. Picha na Vero Ignatus

Meneja wa TANESCO Wilaya ya Karatu Edward Mwakapaju akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo juu ya hali ya utekelezwaji wa mradi wa umeme vijijini REA wilayani humo.Picha na Vero Ignatus

Wananchi wa eneo la Kilimamoja wilayani Karatu wakiwa katika mkutano wa hadhara kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Picha na Vero Ignatus.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...