Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemtaka Mkurugenzi wa Halmauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuhakikisha anahamishia ofisi zake karibu na wananchi ambao wanishi katika mipaka ya halmashauri yake na sio kubaki mjini.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo mji utatanuka na maendeleo yatapatikana na pia kupunguza gharama za kuwahudumia wananchi pindi majanga yanapotokea kwani kuwa nao karibu kutasababisha kutotumia pesa nyingi kuwafuata na wao kupata urahisi wa kufika katika ofisi hizo.

“Rai yangu mkurugenzi mtafute mahala kwingine kwa kujenga ofisi za halmashauri ya wilaya, mahala pengine ambapo ni ndani ya halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na sio ndani ya manispaa, ofisi hii inapaswa iwe nje ya eneo la manispaa, faida yake ni kupanua huduma kuliko kila kitu kufikiria manispaa,” Alisema

Ameyasema hayo alipokwenda kukagua jengo jipya la halmashauri hiyo ambalo lilianza kujengwa mwaka 2012 na kutegemewa kumalizika mwaka 2013 japokuwa bado kukamilika ambapo serikali ilitenga shilingi bilioni 2.3 lakini hadi kufikia katika hatua ya sasa, tayari shilingi bilioni 1.6 zimeshatumika kupitia fedha za Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo (CDG) ambapo kwa sasa imefutwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele) akikongoza ukaguzi wa jengo lililojengwa kwa madhumuni ya kuhamia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele kulia) pamojana na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule wakikagua jengo lililojengwa kwa madhumuni ya kuhamia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 
jengo lililojengwa kwa madhumuni ya kuhamia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...