Rock City Marathon yazidi kuwavutia washiriki wa kimataifa

Zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kufanyika kwa mbio za Rock City Marathon, idadi kubwa ya wanaridha wa kimataifa wameonyesha nia ya kuja nchini ili kushiriki katika mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo wanariadha walioonyesha nia ya kushiriki mbio hizo wengi wanatoka katika nchi za Ethiopia, Ghana, Afrika Kusini, Marekani, Canada, China, Rwanda, Burundi, DRC Congo huku Kenya ikiendelea kuongoza katika orodha ya mataifa ya nje yanaoleta washiriki zaidi katika mbio hizo.

“ Zikiwa zimebaki takribani wiki mbili kabla ya kufanyika kwa mbio hizo tayari zaidi wa washiriki 200 kutoka nje ya nchi wameonyesha nia ya kushiriki mbio hizi na kinachosubiriwa kwasasa ni wao tu kufuata taratibu kupitia Shirikisho la Riadha Taifa (RT). Lengo letu ni kupata washiriki zaidi ya 5000 katika msimu huu,’’ alisema Ngowi katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mapema leo.

“Ni taarifa njema kwetu kuona kwamba baada ya muda mrefu sasa si watanzania bali ulimwengu mzima umeanza kutuelewa nini tunakifanya Kanda ya Ziwa hususani katika jiji la Mwanza…ni ushindi pia kwa sekta ya utalii katika kanda hii.’’alibainisha

Kwa mujibu wa Ngowi, katika kuhakikisha kwamba mbio hizo zinalitangaza vyema jiji la Mwanza, njia ambazo zimekuwa zikitumika kwa wakimbiaji zinahusisha alama muhimu za jiji hilo ikiwemo jiwe la Bismarck lililopo kwenye fukwe ya Ziwa Victoria, makutano ya mzunguko wa samaki (The Vic Fish Roundabout), jengo la Rock City Mall pamoja na Daraja la Furahisha na hatimaye kuishia Uwanja wa CCM Kirumba.
Baadhi ya washiriki wa mbio za Rock City Marathon mwaka jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...