NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuliunga mkono Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiunga na huduma mbalimbali wanazotoa ili liweze kuendelea kutoa gawio kubwa kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi wote hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya rudi nyumbani kumenoga mkoani humo.

Alisema kuwa kupitia gawio ambalo Shirika hilo linatoa kwa Serikali kati ya fedha hizo zinakuja Mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, huduma za maji, shule , ununuzi wa dawa, ulipaji wa mishahara ya watumishi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Ndugu zangu TTCL kumenoga turudi…ukiongeza salio kwenye simu yako hata usipotumia mwezi salio lako liko salama…hivi sasa huduma zao hazihitaji kupanda kwenye mti ndio ufanye mawasiliano, bali popote unawasiliana…hakuna kusema sogea pembeni sikusikii ndio upige simu…hivi sasa hata ukiwa hata porini TTCL inapatikana” alisema.

Mwanri alisema kwa kuunga mkono huduma za TTCL watakuwa nao wajiwekea akiba ya kurudishiwa sehemu ya huduma walizochangia kwa njia ya Serikali kupata gawio na hatimaye kurejesha sehemu ya fedha hizo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba (kushoto) na viongozi wengine wa Shirika hilo wakiwa na bango lenye maneno ya lugha ya Kinyamwezi yenye maana RUDI NYUMBANI KUMENOGA wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo jana mkoani humo. 
1
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(katikati) akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania juu ya huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
2
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwapungia mkono wakazi wa Manispaa ya Tabora wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ilifanyika mkoani humo jana .
4A
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
5A
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipata maelezo  wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo jana.picha na Tiganya Vincent RS TABORA .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...