Halmashauri za Wilaya ya Msalala, Shinyanga (Shinyanga)  Nyang'hwale (Geita), Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji) na Wadau wa Maendeleo ambao ni ACACIA Mining PLC (kupitia Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu) wamesaini hati za makubaliano ya kisheria kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP). 
Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano hayo (Legal Agreement) kijiji cha Ilogi halmashauri ya Msalala, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema katika mradi huo sehemu kubwa ya fedha za mradi zimetolewa na Serikali kupitia wizara ya maji na ACACIA Bulyanhulu Gold Mine Ltd ambapo pia halmashauri hizo tatu zinachangia kiasi cha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi huo kutoka katika makusanyo yake ya ndani. 

Mradi huu utanufaisha jumla ya vijiji kumi na nne (14) kutoka katika Halmashauri za Wilaya tatu ambapo kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga  vijiji viwili ambavyo ni Mwenge na Mahando vitanufaika na mradi huo.

Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akitia saini hati za makubaliano hayo (Legal Agreement) kutekeleza  Mradi wa Pamoja wa Maji ujulikanao kama JOINT WATER PARTNERSHIP PROJECT (JWPP).  Wa kwanza kulia ni Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu. 
 Viongozi wa ACACIA na Serikali wakitia saini hati za makubaliano hayo (Legal Agreement).
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akishiriki kuchimba mtaro katika eneo la Kijiji cha Bushing'we halmashauri ya Msalala ambapo bomba la maji litapita.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...