Na Mathias Canal, WK-Iringa

Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania imeendelea kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na changamoto zinazovikabili vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vinaleta tija kwa jamii.

Hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na kuchukua hatua za kiutawala na kidola kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo waliojihusisha na wizi na ubadhirifu wa fedha katika vyama hivi, mfano; Alayabe SACCOS cha Karatu Mkoani Arusha, Mbinga Teachers SACCOS Mkoani Ruvuma na Ulanga Teachers SACCOS Mkoani Morogoro ambako baadhi ya viongozi na watendaji wamefikishwa mahakamani kwa vitendo vya ubadhirifu.

Vilevile, Kutengeneza mikakati ya kuhakikisha kwamba vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo haviendelei kutengeneza madeni yasiyokuwa na tija kwa jamii na kusaidia kuweka mikakati ya kupunguza madeni ambayo tayari yapo katika vyama vyetu vya ushirika wa Akiba na Mikopo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza umuhimu wa SACCOS nchini wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Sehemu ya wanachama wa vikundi vya akiba na mikopo wakifatilia hotuba ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Willium Vangimembe Lukuvi (Mb) mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani hafla iliyofanyika katika viwanja vya kichangani Mkoani Iringa tarehe 18 Septemba 2018.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...