WAMJW, BUNGENI DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeainisha dawa aina 135 kama dawa muhimu na za kipaumbele cha wizara kwa lengo la kuhakikisha kuwa zinapatikana nyakati zote katika bohari zote za kanda za MSD.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Janii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa ya utendaji ya Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) aliyowasilisha katika kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.

Waziri Ummy alisema tathimini ya upatikanaji wa dawa hizo ni wa hadi mwezi Julai 2018 ambapo ni sawa na asilimia 93 hivyo Wizara yake imeitaka MSD kuongeza idadi ya dawa muhimu 177 na kufikia dawa za kipaumbele 312 ambapo upatikanaji wa dawa hizo ni asilimia 73 kufikia robo mwaka ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019.

“Hali ya upatikanaji dawa muhimu umeimarika kuanzia mwaka 2016/2017 na kufikia asilimia 93 nchi nzima katika mwaka 2017/2018 na hivyo kuweza kufanikiwa katika maeneo mengi na kufikisha dawa moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za afya nchi nzima”.Alisema Waziri Ummy Mwalimu. Aidha, Waziri Ummy alisema MSD imeweza kusambaza dawa moja kwa moja hadi vituo vya kutolea huduma za afya vinavyofikia 5,432 nchi nzima kwa kutumia magari 215 na hivyo kusambaza dawa zenye thamani za shilingi bilionini 600 kwa mwaka kupitia mfumo wa ugavi ulio enea nchi nzima.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua hali ya upatikanaji wa dawa nchini kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini hawapo pichani wakati wa kikao cha kamati ya hiyo kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , katikati aliyekaa ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akichangia mada wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Peter Serukamba akitoa mwongozo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini wakati wa kikao cha kamati ya hiyo kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,wa kwanza kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...