Na Munir Shemweta, Musoma
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumbà na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amepiga marufuku ugawaji viwanja ambayo tayari vimemilikishwa huku wamiliki wake wa awali wakitafutiwa eneo lingine.

Hatua hiyo inafutia kushamiri kwa tabia iliyozueleka kwa baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri kugawa maeneo ambayo tayari yana wamiliki wake kwa watu wengine wenye uwezo na baadaye kuwaahidi wamiliki halali kuwapatia kiwanja kingine.

Mhe Mabula alitoa kauli hiyo wilayani Musoma mkoa wa Mara mwishoni mwa wiki alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi katika Manispaa ya Musoma pamoja na halmashauri za wilaya za Musoma na Butiama wakati wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya februari mwaka 2018.

"Kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri kugawa viwanja 'pandikizi' katika maeneo ambayo tayari yameshamilikishwa kwa mananchi kwani suala hili limekuwa likileta migogoro mikubwa katika sekta ya ardhi" alisema Mabila.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akikagua majalada katika ofisi ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Simiyu Godwin Tumaini mara baada ya kukagua majalada na mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi katika halmashauri ya walaya ya Rorya mkoani Mara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akizungumza na wanakikundi wa Boma la Masai katika wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wana kikundi wa Boma la Masai katika Wilaya ya Serengeti alipopita katika Boma hilo wakati wa ziara yake mkoani Mara mwishoni mwa wiki.
(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...