Serikali imewekeza takribani kiasi cha Shilingi Bilioni 45 kwenye miradi ya maji mkoani Mtwara kwa lengo la kufikisha huduma ya maji mkoani humo kwa asilimia 100.

Akizungumza akiwa ziarani katika Wilaya ya Masasi, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inataka ifikapo mwaka 2020 upatikanaji wa huduma ya maji nchini uwe kwa kiwango cha asilimia 95 mijini, asilimia 90 kwenye miji mikuu ya wilaya na asilimia 85 vijijini.

Profesa Mbarawa amesema ili kufikia lengo hilo mpaka sasa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 45 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji 37 kwenye mkoa wa Mtwara pekee, ambapo mpaka sasa imeshalipa kiasi cha Shilingi Bilioni 25 na Shilingi Bilioni 20 iliyobaki italipwa kwa kadiri hati za malipo zitakapokuwa zinafika wizarani.

Amezungumza hayo mara baada ya kukagua miradi ya maji ya Makong’onda, Chipingo-Mkaliwata na kutembelea chanzo cha maji kinachotumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA).

Profesa Mbarawa amesema kwa sasa mkoa wa Mtawara una jumla ya miradi 37 inayotekelezwa na 4 kati ya hiyo imekamilika, mingine ikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kuahidi itakamilika kwa wakati ili kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mkoa huo.
 Ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata, wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara ukiendelea.
1
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoa msisitizo kwa Jumanne Mackenzie, mkandarasi kutoka Kampuni ya Singilimo Enterprises Ltd akamilishe mradi wa maji wa Makong’onda, uliopo katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara. 
3
Mkurugenzi Mtendaji wa MANAWASA, Mhandisi Nuntufye David akiwa na Waziri wa Maji,  Makame Mbarawa kwenye chanzo cha maji cha Mbwinji.
4
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoka kukagua chanzo cha maji cha Kisimani Newala kilichopo katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.
5
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua maendeProfesaleo ya ujenzi wa mradi wa maji wa Chipingo-Mkaliwata, wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...