IMEELEZWA kuwa Mkoa wa Pwani umefanikiwa kutokomeza  mimba za utotoni  na utoro mashuleni kwa watoto wa kike  kutoka asilimia 18 hadi kushuka kiwango hicho na kufikia  asilimia moja.


Yamesema hayo  na  Mkurugenzi Mkazi  kutoka Taasisi ya Room to Read Peter Mwakabwele  aliyezungumza katika maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11  kila mwaka.

Amesema kuwa taasisi hiyo ya  Room to Read ilijikita  katika Mkoa wa  Pwani  na kuweka mikakati ya kusimamia  haki ya kupata elimu kwa watoro wa kike ambao wanaishi katika  mazingira magumu na kuwapa msaada wa kuwapeleka shule na kuwasimamia katika ngazi ya shule za msingi, sekondari na hata wanao  pata nafasi  ya kuendelea katika ngazi za elimu ya juu.

"Room to Read  tumeweza kufanikisha tunapunguza kasi ya ndoa  za utotoni na utoro mashuleni kwa  kwa watoto wa kike  kwa kuhakikisha  karibu na wazazi  wa mabinti gao na kufuatilia maendeleo yao ya masomo na kuwaelewesha wazazi umuhimu wa mtoto wa kike   kupata elimu" alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa miaka mingi nyuma Mkoa wa Pwani ulikua ukiongoza kwa ndoa za utotoni na utoro shuleni jamabo ambalo lilichangiwa na mila na desturi za unyago wa kuwaweka ndani mabinti na kuwacheza ngoma wakati wenzao wakiendelea na masomo huku wengine  wakiozeshwa baada ya kuchezwa lakini hivi sasa hali imebadilika  kwani mabinti hao wamekuwa wakiongoza kwa ufaulu kwenye mitihani ya kitaifa.

Amekwenda mbali zaidi  kwa kusema kuwa  Room to read wamekuwa wakitumia mbinu za   hali ya juu kwa kuwaweka karibu na kuwasikiliza ikiwemo kuwafundisha stadi za maisha  ili waweze kujiongoza  kielimu na kuweza kukabiliana na  changamoto   mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku na hata familia kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa  Taasisi hiyo ya Room to Read imekuwa ikitoa  bure sare  zashule ,  kuwalipia ada za shule na bweni  kwa wanaoishi  mbali na shule, pia huwapatia chakula na usafiri wa kwenda  na kurudi shuleni pia wapo ambao wamenunuliwa baiskeli ili kuwarahisishia  kwenda shuleni pia wanao wasimamizi na wagamasishaji ambao huwa nao  kwa muda wote ili kuhakikisha lengo la kumkomboa mtoto wa kike linatimia.

Amesema kuwa tayari  mradi huo wa Room to Read umefanikiwa kuwasomesha  wanafunzi wa kike zaidi ya 3500 ambao tayari wamesha hitimu katika viwango vya  ngazi  mbalimbali vya elimu huku wengine wakiwa nje ya nchi wakijiendeleza na  masomo ya elimu ya  juu.

Hivi sasa wanao wanafunzi wanaowasimamaia 8000 ambao wako katika shule ya msingu huku katika sgule za sekondari wako wanafunzi zaidi ya 2,900.

Aidha amezitaja Wilaya ambazo zinanufaika na mradi huo kuwa ni Kibaha, Bagamoyo na Chalinze pia amesema kuwa katika kipindi cha mwaka huu mradi huo umefanikiwa kutanuka baada ya kuongeza kipengele cha kuwawekea somo la biashara ili wale watakaofeli waweze kujiendeleza kibiashara na kujiajiri ili kuweza kujikimu kimaisha.

Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani  Mama Theresia Mbwambo amesema kuwa amewapongeza wadau wa mradi huo  wa Room to Read  kwa kumkumbuka mtoto wa kike na kufanikiwa kumkomboa kielimu.

"Tunatarajia  kwamba hivi sasa watoto wetu wa kike watafanikiwa kusoma vema kama jinsi walivyopanda katika ufaulu kwenye darasa la saba na  mitihani ya kidato cha nne"alisema  Mama mbwambo.

Naye Afisa habari wa Mkoa wa Pwani Alhaji  Maulid Abdul amesema kuwa serikali  ya awamu ya tano ni serikali makini  na kamwe haitovumilia  vitendo vya wazai kuwacheza ngoma watoto wakati wa kipindi cha masomo.

"Hatuzikatai  mila na desturi ni nzuri lakini  ku a  baadhi ya mila inabidi tuziache"alisema 
Mkurugenzi Mkazi  kutoka Taasisi ya Room to Read Peter Mwakabwele akizungumza katika maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike duniani mkoani Pwani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11  kila mwaka. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa mradi  wa Room to Read  Zamaradi  na wa pili kulia ni Afisa elimu mkoa  wa Pwani Alhaj Maulid Abdul nanaliyeketi mwenyw ushungi 
Mrisho Mpoto pamoja na wasanii wengine wakitoa burudani katika maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11  kila mwaka yaliyofanyika mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...