Kaimu mkurugenzi idara ya mwitikio wa kitaifa ,kutoka TACAIDS, Audrey Njelekela akizungumza ,wakati akifungua mkutano uliolenga kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana pamoja na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya,uliifanyika Bagamoyo, Pwani .

NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), imeziasa asasi na mikoa kujiwekea mipango ya kupambana na maambukizo mapya hasa kwenye kundi la vijana wa kike (10-24 )kwani inaonyesha maambukizi yapo juu katika kundi hilo.

Aidha imewataka ,wanaoishi na virusi vya ukimwi kutumia kikamilifu dawa za kufubaza virusi (ARVs), bila kukatisha dozi na wale wasio na maambukizi hayo kupiga vita maambukizi mapya.

Kaimu mkurugenzi idara ya mwitikio wa kitaifa ,kutoka TACAIDS  ,Audrey Njelekela alitoa rai hiyo ,wakati akifungua mkutano uliolenga kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana pamoja na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya,uliifanyika Bagamoyo ,Pwani .

Alisema ,maambukizo mapya yapo  81,000 kwa mwaka,sawa na 6,750 kwa mwezi ambapo asilimia 40 ni maambukizo yaliyopo kwenye kundi la wasichana (10-24) na asilimia  80 ni wanawake wa miaka (15-24 ).
Mkurugenzi wa Sober house Bagamoyo,Karim Banji akizungumza katika mkutano uliolenga kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana pamoja na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya,uliifanyika Bagamoyo, Pwani.

"Tujue mipango tunayofanya tunatafsiri mkakati wa nne
wa kudhibiti ukimwi Tanzania ,na tuna uhakika mikakati yetu ya  ukimwi ya mkoa tulijiwekea vipaombele kwahiyo kulingana na takwimu tulizopewa tunajua ukimwi ulipoegemea "alisema Audrey .
Awali mratibu wa asasi za kiraia kutoka TACAIDS ,Mary Manzawa alisema ,lengo la mkutano huo ni kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi za kiraia na mitandao ya vijana na zinazojishughulisha kuwahudumia watuamiaji wa dawa za kulevya .

Mary alitaja, walioshiriki kuwa ni pamoja na asasi za kiraia ,mitandao ya vyama na asasi zinazojishughulisha kuwahudumia watumiaji wa dawa za kulevya nchini .

Mtoa mada katika mkutano huo ,mratibu wa TACAIDS wa Dar es salaam na Pwani ,Yahaya Mbaga alisema maambukizi yapo juu kwa wanawake zaidi kuliko wanaume.
Alieleza,malengo ya Kitaifa yamelenga kuhakikisha asimilia 90 ya kwanza ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ambao bado hawajajitambua afya zao wawe wamepima ifikapo mwaka 2020.
"Pia wanaoishi na virusi vya ukimwi ifikapo 2020 wawe wameingia katika kutumia dawa za kufubaza VVU na ifikapo mwaka huo asilimia 90 ya ambao wanatumia dawa hizo wawe na virusi vilivyokuwa tayari vimefubaa". Yahaya alitaja lengo jingine, ni kutimiza 000 na ifikapo 2030 kuondoa maambukizi mapya ya UKIMWI,Unyanyapaa na Vifo.

Mmoja wa washiriki katika mkutano huo ,mkurugenzi wa Bagamoyo Sober House ,Karim Banji aliiongeza TACAIDS kwa kushirikisha asasi zinazojishughulisha kuwahudumia watumiaji wa dawa za kulevya.

Hali ya maambukizi ya ukimwi Tanzania kwasasa ni asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.1 ,hali inapungua lakini jamii iendelee kupambana na maambukizi mapya ,na Tanzania bila ukimwi inawezekana".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...