Asteria Muhozya na Rhoda James, GEITA.
Serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Madini imeanza kufanya mazungumzo na nchi ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili iweze kujenga Kiwanda cha Kuchenjua
madini ya Colbat nchini.
Hayo yalibainishwa Oktoba 19,
mkoani Geita na Waziri wa Madini wa Tanzania Angellah Kairuki wakati wa
kuhitimisha ziara ya siku Nne ya Waziri wa Madini wa Kongo (DRC),
Martin Kabwelulu aliyoifanya nchini kwa mwaliko wa Waziri Kairuki.
Kairuki alisema kuwa, nchi ya
Kongo ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat duniani ambapo
asilimia 70 ya madini hayo duniani yanazalishwa nchini humo.Aliongeza kuwa, kwa sasa nchi
hiyo inayo changamoto ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi ikiwemo
ukosefu wa umeme wa kutosheleza kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo.
“Tumekubaliana kuendelea na
mazungumzo na Kongo ili shughuli za uchenjuaji na uyeyushaji wa madini
hayo ufanyike nchini kwa kuwa tumeshaanza kuwekeza kwenye Vinu/viwanda
vya Kuchenjua na kuyeyusha madini mbalimbali. Hivyo, tunataka
wayasafirishe makinikia ya Colbat hapa na tuyachenjue hapa,” alisisitiza
Kairuki.
Akizungumzia matumizi ya madini hayo, Kairuki alisema kuwa, madini ya Colbat yanatumika kutengeneza betri na vihifadhi nishati (capacitor) ambazo zinahitajika sana hususan, kwenye magari yanayotumia umeme.bali na makubaliano ya ujenzi wa
kiwanda hicho, pia Waziri Kairuki alisema kuwa nchi hizo zimekubaliana
masuala kadhaa ikiwemo kuendelea kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa
sekta ya Madini ili kuweza kunufaisha wananchi hasa wale wanaozunguka
maeneo ya migodi.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki na mgeni wake Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (wa pili kushoto) wakimsikiliza Mtaalam Mwelezi Martin Sezinga Akiwaonesha mashine mbalimbali zinazotumiwa katika hatua mbalimbali za uzalishaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu katika mgodi wa mfano wa Lwamgasa.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) na Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Martin Kabwelulu wakiteta jambo baada ya kutembelea mgodi wa Busolwa Mining Ltd unaomilikiwa na Mtanzania, mkoani Geita
Meneja wa Mgodi wa Busolwa Mining Ltd, Flex Adoph akimweleza jambo Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (katikati) wakati alipotembelea katika mgodi huo kujifunza namna mmiliki wa mgodi huo alivyotoka katika uchimbaji mdogo hadi kuwa mchimbaji wa Kati lakini pia kujifunza namna mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchenjuaji na uzalishaji wa madini ya dhahabu. Anayeshuhudia ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki.
Waziri wa Madini wa Angellah Kairuki na Mgeni wake Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu (Wa tatu kushoto) wakiangalia madini ya Dhahabu yanayozalishwa na kuchenjuliwa katika Mgodi wa Nsangano Gold Mine mkoani Geita walipoutembelea mgodi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...