*Asisitiza kwa atakayeenda kinyume na sheria, Serikali itamuwajibisha

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kwamba nchini Tanzania hakuna ubanaji wa uhuru wa vyombo vya habari wala taasisi zisizo za kiserikali.

Amesema jambo hilo linadhihirishwa na uwepo wa jumla ya vituo vya redio 152, ambavyo kati yake ni vituo vitatu tu ndivyo vinavyomilikiwa na Serikali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 24, 2018) katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.“Tunapenda kuwahakikishia kuwa, Serikali ya Tanzania inaongozwa na katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa kujieleza na kupata habari,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba mwananchi yeyote atakayeenda kinyume na sheria, Serikali itamuwajibisha kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Amesema Serikali imeridhia mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na ule wa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Sambamba na kusimamia haki hizo, Serikali imeendelea kutekeleza wajibu wake katika kuiwezesha jamii kuishi salama kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.

Amesema kukuza, kuimarisha na kulinda haki za binadamu ni wajibu wa Serikali na kwa kuzingatia umuhimu huo mwaka 1984 iliingiza sheria ya haki za binadamu katika katiba.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2108. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja wa Mataifa katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi  wa Mashirika ya  Umoja wa Mataifa nchini, katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa Tanzania  katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na  Mratibu Mkaazi wa Mashirika ya  Umoja wa Mataifa  na Mwakilishi wa  Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,  Bw. Alvaro Rodrigues katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Oktoba 24, 2018. Kushoto ni Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...