Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimejipanga kuzuia na kudhibiti madhara yanayosababishwa na machafuko ya kisiasa katika jumuiya hiyo na Bara la Afrika kwa ujumla. Wawakilishi wa nchi hizo wamekusanyika nchini Malawi kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 17 Oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko

Wawakilishi wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi, Magereza na taasisi za kiraia ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa watu 600 wanaoshiriki zoezi hilo lililopewa jina la EX UMODZI CPX 2018 na kaulimbiu ya Afrika ni Amani na Maendeleo (Africa for peace and prosperity).

Katika hafla ya ufunguzi wa mazoezi hayo iliyofanyika leo tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo mji wa Salima takriban kilomita 120 kutoka Lilongwe, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi, Mhe. Evaton Chemulirenji alisema mazoezi hayo ni utekelezaji wa maazimio ya SADC na Umoja wa Afrika (AU) wa kuandaa kikosi cha kukabiliana na machafuko barani Afrika (Standby Force-SF) ambacho kinatakiwa kiwe kimekamilika ifikapo Januari 2019.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ulinzi wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Evaton Chimulirenji akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo na mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko iliyofanyika tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo katika mji wa Salima nje kidogo ya jiji la Lilongwe.Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya SADC yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi ya ulinzi, askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani.

Mratibu wa Program ya Mafunzo yanayofanyika nchini Malawi akieleza mpangilio wa program ya mafunzo hayo kwa ujumla

Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo Meja Jenerali A.B Mhone naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi Mhe. Evaton Chimulirenji (kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi Generali Supini Phiri (kulia) pamoja na Mkuu wa Misheni ya mafunzo hayo, Mhe. Bi. Eunice Lumbia

Sehemu ya viongozi wa kijeshi wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi huo .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...