Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.
Aliyewahi kuwa Msanii wa maigizo wa Kundi la Kaole Ramadhani Ditopile maarufu kama Mashaka amefariki dunia mapema Leo asubuhi katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.
Aidha marehemu Mashaka aliwahi kuonekana kwenye maigizo akishirikiana na waigizaji kama mama Haambiliki,  Cheni, Kisa ,Zawadi akiwa ameshiriki maigizo kama fukuto,sayari, maisha na mingine mingi.
Akizungumza na  wanahabari msanii mwenzie Zawadi amethibitisha kifo hicho na kwa sasa haijafahamika shughuli za msiba zitafanyika wapi.
Na mpaka sasa familia ya marehemu imekaa Kwenye kikao na watatoa taarifa kamili kuhusu maziko ya marehemu mashaka.
Innallillah wahina illah rajuun.
Ramadhani Ditopile "Mashaka" enzi za uhai wake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...