Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

CHAMA cha Wafanyabishara wenye Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA) kimefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania Saleh Kusa Arze ambapo kwa sehemu kubwa mazungumzo yao yamejikita kuangalia fursa za kibishara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Katika mazungumzo hayo nchi ya Libya imeonesha nia ya kuwekeza hasa katika sekte ya nishati ya umeme na kilimo na kuna kampuni ya Libya inataka kuwekeza kwenye mradi wa umeme wa megawati 400. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya Balozi Arze , Kaimu wa Rais wa TCCIA Octavian Mshiu amesema ujio wa balozi huyo kwenye chemba yao umekuwa wa mafanikio makubwa kwani wamezungumza mambo mengi yanayoonesha nia njema katika eneo la biashara kati ya nchi hizo mbili. "Tunashukuru kwa ujio wa Kaimu Balozi wa Libya nchini kwetu.

Kikubwa ambacho tumezungumza pamoja na mambo mengine kuna moja ya kampuni ya nchi hiyo inataka kuja nchini kuwekeza katika mradi wa umeme wa megawati 400.Tararibu bado zinaendelea na pale tutakapokuwa tayari tutatoa taarifa. 

Mshiu pia ametoa rai kwa wafanyabishara nchini kuitumia TCCIA hasa kwa kuzingatia uwepo wao unalenga kuangalia fursa ambazo wafanyabishara wanaweza kuzitumia vema katika kujenga uchumi wa nchi yetu kwa maslahi ya Watanzania wote. "Mwaka huu tunatarajia kusheherekea miaka 30 ya uwepo wa TCCIA. Tumetoa mchango mkubwa na dhamira yetu ni kuendelea kupanua wigo wa fursa za biashara na uwekezaji nchini.
Kaimu Rais wa Chama cha wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) Octavian Mshiu aliyekaa kushoto akisalimiana na Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania Saleh Kusa Arze leo jijini Dar es Salaam baada ya kufika katika ofisi za TCCIA kwa lengo la kujadili masuala ya biashara na uwekezaji.
 Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania Saleh Kusa Arze(kulia) akifafanua jambo kuhusu fursa za uwekezaji baada ya kukutana na Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu (wa kwanza kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania Saleh Kusa Arze(wa pili kulia). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TCCIA Fatma Hamis na wa kwanza kushoto ni Msaidizi wa Kaimu Balozi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...