Serikali imejipanga kuboresha upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa (Green house).  

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoa wa Songea na Iringa ili kuhamasisha na kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujenga vitalu nyumba (Green house) kwenye Mikoa hiyo.

Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali imeamua kuanzisha mradi huo ili kuhakikisha vijana wanafikiwa kwa idadi kubwa na kuwawezesha kupata ujuzi na ajira kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa itakayowawezesha kujipatia kipato.

“Teknolojia hii itawawezesha vijana kulima katika eneo dogo, kupata mazao kwa wingi na kuweza kuyauza, vilevile kutumia eneo hilo kuweza kuajiri vijana wengine kwani asilimia zaidi ya 60% ya watu wanaojiajiri na kujishughulisha inatokana na na mashamba.” alisema Mhagama

Ameongeza kuwa vijana watafundishwa teknolojia hiyo ya kilimo cha kitalu nyumba ili iwawezeshe kuongeza thamani ya mazao watakayozalisha.

Aidha, Waziri Mhagama aliziagiza halmashauri zote kujipanga haraka katika utayarishaji wa miundombinu kwenye maeneo hayo na kuhakikisha vijana wanaandaliwa mapema pamoja na kuanzishiwa Vyama vya Ushirika (AMCOS) kwani  wananchi wapo tayari kuona mradi huo unaanza kufanya kazi mapema.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na viongozi na watendaji (hawapo pichani) alipowasili Halmashauri ya Mufindi, Mkoani Iringa kwa ajili ya ziara ya kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Vijana na Wananchi wa Songea, alipofanya Ziara ya kikazi mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara  Mkoa wa Iringa kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
 Baadhi ya Viongozi na Watendaji kutoka Halmashauri ya Mufindi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa Wilayani hapo kwa ziara ya kikazi kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba. (Kulia ni) Afisa Kazi, Bi. Neema Moshi na Katibu wa Waziri Bw. Raymond Kaseko, wote kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...