Na Mwamvua Mwinyi, FUKAYOSI 
BAADHI ya wakulima kitongoji cha Segwa, kata ya Fukayosi Bagamoyo mkoani Pwani, kinakabiliwa na tatizo la uvamizi wa tembo ambao wameharibu mazao yao kwenye hekari kumi na kuvunja nyumba mbili. 

Akielezea kero hiyo wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dk.Shukuru Kawambwa, katika kata ya Fukayoso, mwenyekiti wa kijiji cha Mwavi,Shabani Mkumbi alisema ,tembo wamekuwa wakitokea hifadhi ya Taifa Saadani na kuvuka mto WAMI na kuingia katika maeneo ya watu kwenye vijiji vya Fukayosi  na Mwavi . 

"Mazao yaliyoharibiwa ni muhogo 
,matikiti,nyanya Maji ,nyanya chungu,maboga , hoho, mananasi, migomba na miwa ." alisema.
 
Mkazi wa Segwa Hassan Kalahuka alisema ,kutokana na tatizo hilo wameamua kuunda kamati ambayo itafuatilia suala la fidia kupitia ofisi ya wilaya kwani wao wamekwama. 

Mmoja wa aliyeathiriwa shamba lake na tembo hao ,Ramadhani Mfaume alielezea ,mbali ya kuharibiwa mazao yake pia gunia zake kumi zimeharibiwa. 

Alibainisha tangu apate hasara hiyo agost 21 mwaka huu hajalipwa kifuta jasho hadi sasa hivyo amemuomba mbunge Kawambwa kuwasaidia. 

Akipokea kero hiyo kubwa, Dk .Kawambwa alisema amepokea taarifa hiyo na ataangalia namna ya kuzungumza na TANAPA, wilaya na wizara husika kuona namna watakavyosaidiwa. 

Akiwa katika kitongoji hicho alifikishiwa bado kuna kero ya ukosefu wa maji safi na salama, wanatumia maji ya visima vya asili ambapo mvua zikikatika wanapata shida zaidi. 

Dk.Kawambwa aliwaambia serikali inaendelea kutatua tatizo la maji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa CHALIWASA, ili hali kupunguza makali ya kero hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...