Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hususani unga wa mahindi na siagi ya karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa sumukuvu ambao ni hatari kwa afya ya watumiaji na wakati mwingine husababisha vifo. 

Mafunzo hayo yanatokana na ripoti ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa bidhaa zitokanazo na unga mchanganyiko na siagi ya karanga uliofanywa na mamlaka hiyo ya mwaka 2015-2018 na kubaini mazo hayo huzalishwa kwa wingi mkoani humo yana dalili ya uwepo wa fangasi na sumukuvu. 

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka amesema kuwa  Mamlaka imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hasa Unga wa Mahindi na Siagi ya Karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Sumukuvu.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy amesema kuwa ugonjwa huo hujitokeza baada ya mlaji kutumia bidhaa zenye vimelea vyake kwa kiasi kikubwa huathiri Ini,kusababisha Saratani na hata vifo kwa watumiaji ambao ni nguvukazi ya Taifa. 

Kessy amesema kuwa mwaka 2015 hadi 2016 na mwaka 2017 hadi 2018 TFDA ilifanya ufuatailiaji wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko na siagi za karanga zilizokuwa zikiuzwa katika soko nchini. 

“Katika ufuatiliji huo ilibainika kuwa bidhaa hizi zilikuwa na dalili ya uwepo wa sumukuvu,hususani katika bidhaa zitokanazo na mahindi na karanga hizi ndizo wajasiliamali wengi wanauza”amesema Bw.Kessy 

Kwa upande wa baadhi ya Wasindikizaji wamekiri kutokuwa na uelewa juu ya sumukuvu kwani awali walikuwa wakisindika Nafaka Kienyeji bila kuchagua mazao ambayo mengine yana dalili za uwepo wa vimelea vya ugonjwa huo. 
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndugu Maduka Kessy akizungumza na wajasiriamali hawapo pichani, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour) na siagi ya karanga yanayofanyika Jijini Dodoma. 
 
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour)na siagi ya karanga wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo 
Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka akitoa ufafanuzi mbalimbali husiana semina hiyo kwa waandishi wa habari ( hawapo Pichani) wakati wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour) na siagi ya karanga yanayofanyika  jijini Dodoma. 
Washiriki wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour)na siagi ya karanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waliokaa kwenye viti kulia ni Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...