Na Chalila Kibuda, Globu, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Mafuta ya Total imeazisha shindano la  Startupper of the Year Challenge kwa ajili  wabunifu wa mawazo ya biashara na kupata  fursa ya ya mtaji pamoja na mafunzo maalumu kwaajili ya uendeshaji wa biashara hizo. 

Shindano hilo la pili kufanyika nchini linaloendeshwa na Kampuni ya Mafuta  ya Total Tanzania na limewalenga vijana wenye mawazo ya biashara na miradi inayoweza kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zao ikiwemo biashara hizo zilitokana na mawazo ziweze kukua.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa Shindano hilo, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya  Total, Thomas Biyong amesema mbali na Tanzania shindano hilo litafanyika katika nchi 40 katika Bara la  Afrika ikiwa ni mpango wa kuinua kazi za ubunifu na kuwa endelevu katika mapinduzi ya biashara.

"Mawaz ya Miradi hiyo itapimwa kulingana na wazo la ubunifu wa asili, umuhimu kwa jamii pamoja na uwezekano wa mradi kuwa endelevu," amesema.

Naye, Mkurugenzi wa Sheria na  Mahusiano wa Kampuni hiyo, Marsha Kileo amesema wabunifu watakaoshiriki wanatakiwa kuwa na biashara ya isyozidi miaka miwili au chini pamoja na wale wenye mawazo mapya.

"Washiriki wetu wa shindano  watakaopatikana  watapata mafunzo maalumu juu ya uendeshaji, uangalizi  na namna ya kuboresha biashara zao,"amesema.

Ametaja masilahi ya washindi watatu watakaopatikana wa Kwanza atapata Kiasi cha Sh.Milioni 30,wa pili Sh. milioni 20 pamoja na mshindi wa tatu atapata Sh.milioni 15 kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi watakayoibuni hapa nchini.
Amesema utaratibu wa kutuma katika tovuti ya Total ambayo imefunguliwa Oktoba Tisa na kuisha Novemba Mwaka huu.

Shindano la kwanza lilifanyika mwaka 2015 ambapo Iddi Kalembo kutoka Mtwara aliibuka mshindi kwa mradi wake wa upigaji picha kwa njia ya simu hasa vijijini.

Mshindi wa tatu Krantz Mwantepele ambaye ndiye mlezi wa shindano hilo amesema vijana wanatakiwa kuwa wabunifu kwani kwa mawazo yao wanaweza kushinda na kupata mtaji wa kuendeleza Biashara zao.
Amesema aliposhinda nafasi ya tatu amepata fursa za kutosha ikiwa ni pamoja na kuendeleza biashara yake.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Total Thomas Biyong akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa shindano la Start upper of the year Challenge uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total Marsha Kileo akizungumza kuhusiana jinsi uwasilishaji wa mawazo yao katika tovuti yao kwa muda uliowekwa.
Mlezi wa Shindano hilo Krantz Mwantepele akizungumza kuhusiana na ushindi wake wa awamu ya kwanza na namna akuvyonufaika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...