MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.65 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.32 na kuongeza kuwa ukusanyaji wa mapato hayo umekuwa ukiongezeka kila mwezi.

“Katika mwezi Julai, 2018, TRA ilikusanya jumla ya shillingi trillioni 1.20 sawa na ukuaji wa asilimia 9.20, mwezi Agosti, 2018 jumla ya shilingi trillioni 1.27 zilikusanywa ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.86 wakati mwezi Septemba, 2018 mamlaka ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.36 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.65,” alisema Kayombo.

Kayombo amewashukuru walipakodi wanaoendelea kulipa kodi zao kwa hiari na wakati na amewahimiza wale wote ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo na wale wenye changamoto mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za TRA mikoani na wilayani ili kuonana na mameneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Aidha, Kayombo amesema TRA inaendelea na zoezi la kupokea maombi ya misamaha ya riba na adhabu katika malimbikizo ya madeni ya kodi za nyuma ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa jumla ya walipakodi 1,950 wamewasilisha maombi ya kusamehewa riba na adhabu ambayo yanafikia jumla ya shilingi bilioni 185.4.

“Mwitikio wa walipakodi kuomba msamaha wa wa riba na adhabu ni mkubwa na unaridhisha na kuna baadhi ya walipakodi waliowasilisha maombi ambao wameshapewa majibu na wengine wako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa maombi yao. Hivyo, nachukua fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara ambao hawajawasilisha maombi wawahi kuwasilisha maombi hayo kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.

Mkurugenzi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kuwaasa wale wote wanaojishughulisha na vitendo vya kugushi risiti za kielektroniki za EFD nchi nzima hasa maeneo ya Kariakoo, kuacha mara moja kwa sababu wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi mitatu kwa mwaka wa feda 2018/2019. Kulia ni Meneja wa huduma na elimu kwa mlipakodi Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Gabriel Mwangozi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kulia ni Meneja wa huduma na elimu kwa mlipakodi Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Gabriel Mwangozi na kushoto Meneja wa huduma na elimu kwa mlipakodi Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA).
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...