*Waziri wa Mambo ya Ndani asema tukio 
la MO si kigezo cha kuingiwa hofu kuwekeza nchini 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

SERIKALI imewahakikishia Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba Tanzania ni nchi usalama ya kuwekeza na tukio la kutekwa kwa mfanyabiasbafa Mohammed Dewji lisiwape hofu. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema si sawa kutumia tukio la kutekwa kwa MO kama kigezo cha kuifanya Tanzania kuonekana si mahala na kuwahakikishi nchi iko salama na kufafanua hakuna nchi iliyosalama zaidi ya Tanzania. 

"Mimi niwahakikishie Watanzania na dunia kwa ujumla kwamba nchi yetu iko salama na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara kwetu ni geni na limetushutukiza.Hata hivyo nitoe rai nchi ya Tanzania ni salama na wawekezaji wake kuwekeza tu,tuko salama sana," amesema Waziri Lugola. 

Ametoa kauli hiyo baada ya waandishi wa habari kutaka kufahamu iwapo tukio la kutekwa kwa MO Dewji linaweza kusababisha kuwatia hofu wawekezaji na kutumia nafasi hiyo kuhakikisha nchi iko salama kwa uwekezaji. 

Waziri Lugola amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imeampa kuhakikisha nchi iko salama na kusisitiza vyombo vya ulinzi na usalama viko imara."Wapi ambako wawekezaji watakwenda kukawa salama zaidi ya Tanzania.Watakuja tu na sababi nchi yetu tukio salama sana na inafaa kwa wawekezaji kuja kuwekeza.Wasiwe na hofu," amesema Lugola.

AONYA, ATAKA MITANDAO ITUMIKE 

Waziri Lugola amewataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu kwani kinyume na hapo wataitumia kuleta uchochezi, hofu na udanganyifu.“Wananchi wawe makini na kwani umakini utasaidia kuondoa mkanganyiko.Taarifa zozote za matukio ya uhalifu zitatolewa na Jeshi la Polisi,”amesema . 

Ametoa onyo kwamba asitokee mtu yoyote anayetaka kutumia matukio yanayojitokeza kama mtaji wa kisiasa au kujipatia umaarufu. 

Asitokee mtu yoyote ambaye atatumia matukio hayo kuaminisha mataifa mengine kwamba nchi haiko salama. Akitokea mtu wa aina hiyo ajue atakamatwa na atachukuliwa hatua,”amesema.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani ),alipokuwa akizungumza nao leo mchana katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya ndani kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo tukio la utekwaji wa Mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji,ambapo pia amewaonya watu kutotumia mitandano ya kijamii kupotosha kwa kuiaminisha Dunia kuwa Tanzania si mahali salama pa kuwekeza,kwani atakabainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akizungumzia usawa ambao Jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola katika kushughulikia matukio yoyote yanayotokea na kwamba Watanzania wote wana haki sawa hakuna cha tajiri au masikini kwani kuna dhana imeanza kujengeka kuwa matajiri wanapopatwa na tatizo wanaangaliwa zaidi 
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola alipokuwa akizungumza nao leo mchana katika ofisi ndogo za Wizara ya Mamo ya ndani kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo tukio la utekwaji wa Mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji.
Waziri Kangi Lugola akijibu baadhi ya maswali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...