Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam.
Serikali imeagiza kuchunguzwa kwa vitendo vya ukatili hasa ukeketaji kwa watoto wachanga unaondelea kufanyika nchini kwa baadhi ya makabila yenye mila za ukeketaji wamebadili mbinu na kuanza kukeketa watoto wachanga kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo wakati akiongea na vyombo vya habari katika mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana masuala ya ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.

Naibu Waziri Ndugulile amesema kufuatia jamii hizo kubadili mwenendo wa ukeketaji na Serikali kubaini mbinu hizo amesisitiza agizo lake alilolitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika Mkoani Arusha la kuwataka madaktari wote nchini kufanya uchunguzi kwa watoto wote wachanga ili kubaini kama watoto hao wamefanyiwa ukatili kwa kukeketwa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa utafiti unaonesha kuwa takwimu za mimba za utotoni bado ziko juu Nchini nakutaja mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni kuwa ni Katavi 45%, Tabora%, Morogoro 39%,Dodoma 39%, na Shinyanga 34%.

Aidha ameamuagiza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushirikiana na Idara Kuu ya Afya kuona namna bora ya kupamba na vitendo hivyo na kuhakikisha vitendo vya ukeketaji kwa watoto wachanga vinakomeshwa nchini.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kutoka  vyombo mbalimbali vya habari wakati wa mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
 Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto John Jingu akielezea jitihada za Wizara katika kukabiliana na vitendo vya uaktili kwa watoto wa kike kwa vyombo vya habari wakati wa mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
 Baadhi ya Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari na wadau wa mtoto wa kike wakifuatilia mdahalo wa Kitaifa kuliofanyika jijini Dar es Salaam   kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto John Jingu akiwa katika picha na viongozi nz wajumbe wa Baraza la watoto la taifa na wadau wa maendeleo na ustwi wa Mtoto mara baada ya kumalizika kwa mafunzo kwa watoto kuhusu mimba na ndoa za utotoni yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kitengo cha Mawasilianio WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...