Na Said Mwishehe, Glogu ya jamii

UCHAGUZI wa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam umeshindwa kufanyika kutokana na sabababu mbalimbali ikiwemo ya mvutano wa pande mbili kati ya wajumbe wanaoshiriki uchaguzi huo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na wa vyama vya upinzani.

Wajumbe wa uchaguzi huo ni madiwani na wabunge wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo baada ya mvutano mrefu ulioanza tangu ajenda ya uchaguzi ilipowasilishwa mezani na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Spora Liana.Mwenyekiti wa uchaguzi huo alikuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.

Mchakato wa uchaguzi huo ulianzaa saa nne asubuhi na kuendelea hadi saa nane mchana.Baada ya malumbano ya muda wote huo ilitolewa hoja ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.Mbunge wa jimbo la Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jisnia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile alitoa hoja ya kuahirishwa uchaguzi huo.

"Mheshimiwa Mwenyekiti na Mkurugenzi pamoja na wajumbe wengine naomba busara itumike...tuahirishe uchaguzi huu hadi siku nyingine.Kwa namna hali ilivyo leo hii hatutafanikiwa.Kila upande utataka kushinda na matokeo yake hatutafika mwisho.Hivyo tuahirishe," amesema 

Dk.Ndugulile wakati anatoa hoja hiyo.Baada ya kuiwasilisha wajumbe waliiunga mkono hoja hiyo.Hivyo uchaguzi huo umeahirishwa hadi hapo utajapotangazwa tena.

KABLA UCHAGUZI KUAHIRISHWA
Baada ya wajumbe wenye sifa ya kushiriki uchaguzi huo wapatao 23 kuingia ukumbini dalili za malumbano zilianza kuonekana mapema kutoka kwa baadhi ya wajumbe ambao ni madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Madiwani wa CCM na wa upinzani ambao ni Chadema na CUF walikuwa wakishindana kwa hoja.Kuna wakati utulivu uliotoweka na kusababisha kelele kuibuka mara kwa mara kiasi cha Mwenyekiti wa uchaguzi kutumia rungu lake kutuliza madiwani.

Mjadala mkali uliibuka baada ya Mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuwa uchaguzi huo kuna jina moja la mgombea wa nafasi ya Naibu Meya ambaye ni wa CCM Mariam Rulida.Mkurugenzi hiyo wa Jiji hilo alisema jina la mgombea wa CUF liliondolewa baada ya aliyekuwa anagombea nafasi hiyo kujiuzulu nafasi zake zote na kisha kujiunga CCM.

Hata hivyo baada ya majibizano ya muda mrefu walikubaliana haina tatizo uchaguzi ufanyike.Baada ya kukubaliana ikaibuka hoja nyingine iliyowasilishwa na madiwani wa upinzani kwa kutaka kuwe na kura ya ndio na kura ya hapana.

Eneo hilo nalo liliibua utata baada ya madiwani kutaka upigaji wa kura ufanyike mbele ya wajumbe na watakaopiga kura ya hapana wawe na wakala wao na wale watakaopiga kura ya ndio nao wawe na wakala.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Jiji ambaye ndio msimamizi wa uchaguzi huo alisema kura ni siri ya mpiga kura na hivyo lazima utaratibu 
ufuatwe.Hivyo kukaibuka malumbano yaliyochukua muda mrefu.

Madiwani wa upinzani wao walitaka kura isiwe siri kwani kwa idadi yao inatosha kupiga kura ya hapana.Pia hoja nyingine ni 
muongozo wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya uliodaiwa ni wa Wizara uliowasilishwa na ya wajumbe wa upinzani.Muongozo huo nao uliiibua utata mkubwa huku baadhi ya wajumbe wakionesha kutokuwa na imani nao kwa kuwa haukutolewa na Mkurugenzi wa Jiji

Hata hivyo kwa namna ambavyo malumbano hayo yalitawala na wapinzani kuonesha hawana imani na Mkurugenzi wa Jiji ,hali hiyo nayo iliyozidisha mjadala kwa pande zote mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...