WAFANYAKAZI wa benki ya TIB Corporate  wamtembelea Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa jijini Dar es Saaam leo.

Uamuzi wa wafanyakazi wa benki hiyo kwenda MSD nimwendelezo wa kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja kwa namna ya kutembelea wateja wao kwaajili ya kutoa shukurani kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa amewashukuru benki hiyo kwani wamefanya kitu cha tofauti pia amewatia moyo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na kujituma.
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD)  mwenye tisheti ya bluu leo mara baada ya kutembelewa na wafanyakazi hao ofisini kwake.
Mfanyakazi wa benki ya TIB Corporate akiangalia boksi la dawa mara baada ya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa kuwaonesha jinsi bohari hiyo ilivyo.
Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa  akiwaonesha baadhi ya maboksi ya dawa wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakiwa  kutembelewa na wafanyakazi hao  jijini Dar es Salaam na kuangalia mteja wao anavyofanya kazi.
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakitembelea bohari ya dawa (MSD)mara baada ya mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika Oktoba kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...