Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, kupitia mpango wake wa Pamoja na Vodacom leo wametoa msaada wa vifaa vya kusomea kwa Wanafunzi zaidi ya 150 wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo iliyoko Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Elimu bora kwa wote ni moja kati ya nguzo kuu za asasi ya Vodacom Tanzania Foundation hivyo msaada huu wa nyenzo za kujifunzia pamoja na vifaa mbalimbali vya elimu kwa ajili ya wasioona pamoja na wale wenye uoni hafifu utaisaidia shule kukabiliana na matakwa mbalimbali ya kuhudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Upatikanaji wa vitabu vya nukta nundu (vitabu maalum kwa Wasioona) pamoja na maandiko mengine, ni hafifu na msaada huu utasaidia katika kupunguza ukubwa wa tatizo hili. Msaada huu kutoka kwa Wafanyakazi wa Vodacom unahusisha mashine kumi na karatasi maalum za kuchapia maandishi ya nukta nundu (Maandishi maalum kwa Wasioona), viti, faili za plastiki (maalum kwa ajili wasioona), vifaa hivi vitasaidia zaidi ya wanafunzi 67 wenye shida ya macho katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. 

Kwa sasa Walimu wataweza kuandaa lesoni na vifaa maalum vya kufundishia kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu. Zaidi ya hayo, Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wamejitolea nguo, sabuni na vyakula mbalimbali ili kuwasaidia wanafunzi hao.

Akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani George Lugata alisema, “elimu ni haki ya msingi na kipengele muhimu cha malengo endelevu ya milenia, tunatambua mchango muhimu wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko katika kuwalea Watoto walio pembezoni wenye ulemavu kwa kuwapa elimu bora inayoendana na mahitaji ya wanafunzi.” 


Kamishna msaidizi watu wenye ulemavu, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, ajira na watu wenye ulemavu, Beatrice Fungamo (Kushoto) akipokea moja ya mashine maalum za kuandikia maandishi ya nukta nundu (Braille) zilizotolewa jana na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiongozwa na mkurugenzi wa kanda ya Pwani George Lugata, vifaa hivyo vitaleta ufanisi katika kutoa elimu bora kwa wasioona na wale wenye uoni hafifu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...