Na WAJMW-DODOMA
Watu wenye matatizo ya macho takribani 700 wamefanyiwa uchunguzi na kati ya hao wagonjwa 300 waliobainika kuwa na matatizo ya macho wamefanyiwa upasuaji na kurejeshewa hali ya kuona vizuri.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Mpango wa Huduma za Macho kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Bernadetha Shilio wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya siku ya afya ya macho duniani kilichofanyika mapema leo katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma.
“Siku ya afya ya macho duniani ina lengo kuu la kuhamasisha utekelezaji wa dira ya kimataifa ya kutokomeza upofu unaozuilika ifikapo mwaka 2020, na kutathmini haki ya kuona kwa wote ambapo mwaka 2003 serikali ya Tanzania iliungana na mataifa mengine duniani katika kutekeleza azimio hilo”. Alisema Dkt. Shilio
Dkt. Shilio amesema Serikali ya Tanzania inashirikiana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya afya ya macho ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii, kutoa huduma za uchunguzi wa macho pamoja na kufanya upasuaji kwa wagonjwa ambao watabainika kuwa na matatizo.
Pia Dkt. Shilio ameiasa jamii ya kitanzania kuzingatia kanuni sahihi za utunzaji wa macho ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza na kusababisha uono hafifu na kupelekea upofu. 
“Matumizi ya rangi na kope bandia kwenye ukingo wa macho, kuvaa miwani bila kupima, kutumia dawa za mgonjwa mwingine wa macho bila ushauri wa daktari, kutokula vyakula bora vyenye virutubisho na kutokua na tabia ya kupima macho angalau mara moja kwa mwaka vimetajwa kuwa visababishi vikubwa vya kuathiri afya ya macho” alisema Dkt. Shilio.
 Mtaalam kutoka Taasisi inayojishugulisha na afya ya macho ONA  Bi. Haika Urasa kulia akitoa miwani ya kusomea kwa mmoja wa wakazi wa Dodoma aliyefika kupata huduma ya afya ya macho katika viwanja vya Nyerere Square wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.
 Mtaalamu wa magonjya yasiyoyakuambukiza Dkt. Nleminyanda Hezron katikati akitoa huduma za kupima sukari kwa baadhi ya wakazi wa Dodoma kupata huduma hizo katika viwanja vya Nyerere Square wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.
 Moja ya Wataalam  wa Afya ya macho akitoa elimu juu ya afya ya macho kwa baadhi ya wakazi wa Dodoma waliofika  katika viwanja vya Nyerere Square wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo.

Baadhi ya wakazi wa Dodoma waliofika  katika viwanja vya Nyerere Square  wakisubiri kupata huduma ya afya ya macho na magonjwa yasiyoyakuambukiza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho yaliyofanyika mkoani humo leo. PICHA NA WIZARA YA AFYA

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...