WAZIRI wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kutoficha vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) wakati wa usajili wa wananchi wanaohitaji kuunganishwa na huduma hiyo. 

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, aliyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga ambapo alizindua huduma ya umeme katika kijiji cha Magaoni na Kibiboni vilivyopo wilayani Mkinga na Kijiji cha Tingeni na Kwabota vilivyoko wilayani Muheza. 

“ Ni marufuku kwa mkandarasi kuficha vifaa vya Umeta wakati wa usajili wa wananchi, hakikisheni vifaa hivi vinakuwepo na mwananchi awe huru kuchagua kama anahitaji kuunganishiwa umeme kwa kutumia UMETA au kuingia gharama ya kutandaza nyaya ndani ya nyumba yake,”alisema Dkt Kalemani. 

Alisema kuwa, kila mkandarasi amepewa vifaa vya Umeta 250 kwa kila eneo lake la mradi hivyo wana wajibu wa kuhakikisha kuwa, wananchi wanafahamu uwepo wa vifaa hivyo ili kuwapunguzia gharama za kutandaza nyaya ndani ya nyumba. 

Katika mikutano yake na wananchi, Dkt Kalemani aliwahamasisha kutumia vifaa hivyo kwani Mkandarasi anapomaliza idadi ya Umeta aliyokabidhiwa na Serikali, vifaa hivyo huuzwa kwa bei ya shilingi 36,000 . 
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuanza kupatikana kwa umeme katika Kijiji cha Magaoni wilayani Mkinga mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mbunge wa Mkinga, Dunstan Kitandula. 
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (mwenye kipaza sauti) akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kibiboni wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga ambapo pia alizindua huduma ya umeme katika Kijiji hicho. 
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) na Mbunge wa Mkinga, Dunstan Kitandula wakipongezana mara baada ya Mbunge huyo kukabidhiwa vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) vitakavyotumika kuunganishia umeme wananchi wa Kijiji cha Magaoni wilayani Mkinga mkoani Tanga. 
Baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magaoni mkoani Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...