Na Frankius Cleophace, Serengeti.

Wasichana zaidi ya  400 (Mianne) wa shule za sekondari wilayani Serengeti Mkoani Mara wamepatiwa elimu ya kupinga Ukeketaji kwa mtoto wa kike pamoja na elimu ya Afya ya Uzazi na utunzaji wa Mazingira kwa lengo la kukomboa Mwanamke huku wengine 1160 wakitarajia kupatiwa elimu hiyo. Hayo yamebainishwa na Frida Mollel ambaye ni  Meneja Idara ya Maendekeo ya jamii kampuni ya  Singita Grumeti Fund iliyopo wilayani  Serengeti  Mkoani Mara  katika viwanja shule ya Msingi Makundusi baada ya kutoka Shule ya Msingi Natta kwa kukikbia mbio fupi.

Frida amesema kuwa wao kama kampuni wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na wanakijiji kutoka vijiji 21 vinavyozunguka hifadhi ya Ikorongo Grumeti Reserves ili kuendelea kutunza mazingira na jamii kuondokana na ujangiri ili kulinda hifadhi pamoja na wanyama ili kunufaisha kizazi kijacho.
Meneja Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Mollel akitoa elimu ya kupinga Ukeketaji na mila kandamizi kwa wasichana pamoja na wanawake katika viwanja vya shule ya Msingi Natta wilayani Serengeti mkoani Mara.

Licha ya kutolewa kwa elimu ya kutunza mazingira Frida amesema kuwa wanafunzi hao wamepewa elimu ya kupinga suala zima la ukeketaji na mila kandamizi ambazo zinazidi kundamiza mwanamke pamoja  na msichana mpaka kushindwa kutimiza ndo zake ambapo elimu hiyo imeanza kutolewa tangu mwaka jana lengo ni kukomboa mwanamke.

“Mwaka jana tuliweza kukutana na wasichana wakatupa changamoto zinazowakumba kipindi cha ukeketaji na mwaka huu Serengeti kulingana na mila na desturi watakeketa sasa tumeona tutumie fursa hii kutoa elimu ili kukomboa mtoto wa kike ukiangalia pia kuna wanawake ambao wametoka nje ya nchi ya Tanzania kwa maana ya Afirika kusini na Marekani ili kutuunga mkono lengo ni kutoa hamasa kubwa kwa mabinti hao pia wameweza kukimbia mbio fupi ni wasichana hao alisema Frida.” alisema Frida.
Rnonda Vetere Kutoka New York City Marekani akiongea na wanafunzi wa shule za sekondari kuhusu mwanamke kijiamini ambapo amewasihi kudhubutu na kujiamini kwa lengo la kufanikiwa huku wakiendelea kutoa elimu juu ya kupinga mila kandamizi.

Katika kutoa elimu hiyo na kutoa hamasa kwa mabinti hao baadhi ya washiriki ambao wamekuwa wakitoa elimu wametoka nje ya Nchi huku baadhi yao wakitoka  Afrika Kusini, na Marekani  Rnonda Vetere kutoka New york City Nchini  Marekani  amezidi kuhamasisha wanawake Nchini Tanzaniakuendelea  kujiamini na kudhubutu kwa lengo la kupata mafanikio ili kuendeleza mapinduzi katika kutokomeza Mila kandamizao ukiwemo Ukeketaji kwa mtoto wa kike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...