Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam katika kozi ya uhasibu wameaswa kujinoa vizuri katika mitihani ya Bodi ya Uhasibu Nchini (NBAA) ili waweze kufanya vizuri katika mitihani hiyo ambayo itaanza hivi karibuni.

Akizungumza na wanafunzi wa wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Afisa Mitihani wa Bodi ya Uhasibu (NBAA) Humphre Sympholian amesema kuwa mitihani ya bodi sio migumu kinachotakiwa kwa wanafunzi kujiandaa vizuri ambapo wanaweza kufanya vizuri.

Amesema kuwa kwa wale wanaofanya kazi katika kipindi kilichobaki waweze kuomba ruhusa ya kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo na kuweza kupata cheti mahususi kwa ajili ya uhasibu (CPA).
Sympholian amesema kuwa mitihani hiyo wamekuwa mtihani wa bodi hiyo hauna upendeleo hivyo kila mtu atapata alichokipanda katika kujiandaa kwake na huo mtihani.

“Hatuna upendeleo kwani wanaosimamia sio ndio wanaosahihisha na kusahihisha huko hakuna majina ya wanafunzi kilichopo ni namba tu ambapo hawezi kupenya mwanafunzi wa kwa upendeleo”amesema Sympholian. 

Mhasibu na Mwalimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Victirius Kamuntu amesema kuwa wanafunzi wake wamejiandaa na kuwa na imani kuwa mitihani ya bodi watatafanya vizuri.
Amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe katika mitihani ya bodi hiyo kwa wanafunzi chuo hicho wamekuwa wakifanya vizuri hivyo kukutana na watu wa bodi kunawafanya kuongeza juhudi ya kufikia malengo.
 Afisa Mitihani wa Bodi ya Uhasibu (NBAA) Humphre Sympholian akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuhusiana na mitihani ya Bodi itayofanyika hivi karibuni alipokutana na wanafunzi hao katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mitihani wa NBAA, Rebecca Siame akieleza sheria zinazotumika na Bodi ya NBAA katika usimamizi wa Mitihani na mwanafunzi atakayebainika kufanya udanganyifu matokeo yake kufutwa wakati alipokutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wanaojiandaa na Mitihani ya Bodi ya Uhasibu Nchini(NBAA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...