Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka wananchi wa Mikoa Nyanda za Juu Kusini kushiriki maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali na huduma za mitaji yatakayo fanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya kuanzia tarehe 19 hadi 23, Octoba, 2018 ili kujionea fursa za uwezeshaji kuelekea katika uchumi wa viwanda.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam kuwa maonyesho hayo hayo ni ya bidhaa za wajasiriamali na huduma za mitaji na yatafunguliwa na Waziri Kassim Majaliwa Octoba 20, 2018 na ambayo yanalenga kunadi fursa za uwezeshaji.

“Maonyesho haya yatawezesha upanuaji wa wigo wa masoko ya wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za mikono kwa kutumia mali ghafi za Tanzania,” na hiyo inatoa hamasa kwa wananchi kujikita katika viwanda vidovidogo.

Baraza limeshirikiana na Mifuko ya Uwezeshaji, Vikundi vya kifedha na program za serikali za uwezeshaji kuandaa maonyesho hayo na yatafungwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Bw. Charales Mwijage, aliongeza kusema,Bi. Issa. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Bengi Issa wa pili kushoto akisisitiza jambo wakati walipokuwa akizungumza kuhusu maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji, Taasisi za Vikundi vya Kifedha na program za uwezeshaji yatakayo fanyika Viwanja vya Ruanda Nzovwe Mbeya kuanzia tarehe 19 hadi 23 octoba 2018, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Bw. Nicomed Bohay, kushoto mwakilishi wa IR-VICOBA, Bi. Augustina Mosha na wa pili kusho ni Mwenyekiti wa VICOBA FETA,Bw. Filbert Sambali. (Picha na Mpiga Picha wetu, Dar es Salaam).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...