Na Estom Sanga-Zanzibar

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Ksiwani Unguja Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud amepongeza jitihada zinazofanywa na Mfuko huo katika kutekeleza maelekezo ya serikali ya kusaidia jitihada za kuwandolea kero ya umaskini wananchi. 

Bwana Mahmoud ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema TASAF imekuwa kielelezo sahihi na cha kujivunia katika kutekeleza wa sera za kupambana na umaskini kwa kushajihisha wananchi kujiletea maendeleo kwa kutumia nguvu na raslimali zilizoko kwenye maeneo yao. 

Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kianga unatekelezwa na Wananchi kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF kupitia utaratibu wa Mfuko huo wa kuendeleza miundombinu ya Afya,Elimu na Maji kwenye maeneo ya Walengwa. 

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema miradi iliyoibuliwa na Wananchi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF imeleta mageuzi makubwa katika maeneo mengi ya visiwa hivyo kufikia hatua ya baadhi yao kuzalisha bidhaa za kilimo kama vitunguu maji na hivyo kujiongezea kipato na kuukimbia umaskini uliokuwa unawakabili. 

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga amesema tangu Mfuko huo ulipoanzishwa na Serikali, umetoa mchango mkubwa katika kusaidia jitihada za kuboresha maisha ya wananchi huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo yametokana na sera sahihi za kupambana na umaskini zinazoratibiwa na serikali. 

Bwana Mwamanga amesema TASAF imekuwa ikizingatia kwa kina maelezo ya Serikali yanayotilia mkazo pamoja na mambo mengine umuhimu wa wananchi wakiwemo Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuondokana na adha ya umaskini na kujiongezea kipato chao. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Serikali kupitia Mfuko huo imeamua kubosheresha kuboresha zaidi utekelezaji wa Mpango huo ili uweze kuwafikia wananchi wote wanaokabiliwa na Umaskini nchini huku msisitizo ukiwa ni kuibua shughuli za uzalishaji mali kwa kufanya kazi na kisha kulipwa kulingana na kazi watakayokuwa wameifanya. 

Kwa Upande wao wananchi wa shehia ya Kianga wameishukuru Serikali kwa kuuwezesha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo kwenye shehia yao ukiwemo mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachowapunguzia adha ya kufuata huduma hiyo mbali na eneo lao.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akihutubia wananchi wa Shehia ya Kianga,wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar (hawapo pichani) baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha Afya unaotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi wa eneo hilo.

 Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi ,Unguja Bw. Ayoub Mohamed  Mahmoud (aliyesisima nyuma ya meza) akiwahutubia wananchi wa Shehia ya Kainga baada ya kukagua ujenzi wa jengo la kituo cha Afya cha shehia hiyo unaojengwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi.
 Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Bw. Mahmoud akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.Mwamanga na maafisa wa serikali baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya-Kianga (nyuma yao)
 Baadhi ya wananchi wa Shehia ya Kianga kisiwani Unguja wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga( hayupo pichani) baada ya kukagua jengo la kituo cha Afya kinachojengwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi.
 Sehemu ya jengo la Kituo cha Afya Kianga katika mkoa wa Mjini Magharibi kinachoendelea kujengwa TASAF na Wananchi wa eneo hilo ambacho kitapunguza tatizo la kufuata huduma za Matibabu mbali na eneo lao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...