Wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamewasili leo Musoma, mkoani Mara kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo kwa njia ya mkoba pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu wa hospitali za rufaa za mikoa nchini.

Lengo la ziara hii ni kuwaongezea ujuzi wataalamu wa hospitali za rufaa kupitia wataalamu wabobezi wa muhimbili ikiwa ni kutekeleza mpango mkakati wa MNH wa kuhakikisha inazitembelea hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ambao pengine wangepewa rufaa kwenda kupata huduma za kibingwa Muhimbili.

Baada ya timu ya wataalamu 14 kuwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma mkoani Mara, ilipokelewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Joachim Eyembe na hakusita kueleza furaha yake kwa ujio wa watalaamu hao wabobezi ambao watawajengea uwezo wataalamu wenzao katika maeneo ya upasuaji wa pua, koo, masikio na usingizi na kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa wa Mara.

“Kwa kweli tuna furaha kubwa kwa ujio wenu kwani tunaamini tutanufaika katika ushirikiano wetu wa kutoa huduma bora kwa wananchi wa Mkoa wa Mara. Naamini tutafanya kazi ambayo itakidhi mahitaji ya wananchi wa mkoa huu,” amesema Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo. Dkt. Eyembe.



Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Musoma mkoani Mara, Dkt. Joachim Eyembe akiwakaribisha wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kuwasili leo Musoma kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa kushirikiana na wataalamu wenzao wa hospitali hiyo.
Wataalamu wa afya wa Muhimbili na wa Hospitali ya Rufaa Musoma wakimsikiliza Mganga Mfawidhi, Dkt. Eyembe leo wakati akiwakaribisha wataalamu wa MNH.
Wataalamu wa Muhimbili na wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma wakijadiliana jambo baada ya kuwasili kwenye hospitali hiyo leo.
Baadhi ya wataalamu wa Muhimbili wakiwa safarini kuelekea Musoma mapema leo asubuhi.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...