Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WaZIRI wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi hadi sasa linawashikilia watu 20 kwa ajili ya kuwahoji na kuchukua ushahidi utakaowezesha kupatikana kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na vyombo vya habari kuhusu matukio mbalimbali yakiwamo ya utekaji watu.

Waziri Lugola amesema kwamba Jeshi la Polisi nchini wanaendelea  kumtafuta Mo Dewji na kuwasaka walimtoka.
"Watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na kutoa taarifa ambazo zitasaidia kupata ushahidi ambao utasaidia kumpata Mo Dewji," amesema Waziri Lugola.
Pia amesema pamoja na kushikiliwa kwa watu hao kwa ajili ya ushahidi wa kufanikisha kupatikana kwa Mo na kwamba watakaohojiwa na ikibainika wanastahili kuachiwa basi iwe hivyo ndani ya saa 24.
"Nimetoa maagizo kwa Polisi kuhakikisha walioshikiliwa wanahojiwa na ndani ya saa 24  kama hakuna sababu ya kuendelea kushikiliwa waachiwe," amesema.
Alipoulizwa sababu za kutekwa kwa Mo,Waziri Lugola amejibu kuwa kwa sasa hawajui sababu za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo na kwamba atakapopatikana basi sababu zitajulikana pamoja ba waliomteka nao watatoa sababu.Alipoulizwa ni hatua gani zinafanyika kuzuia matukio hayo yasitokee amejibu Polisi wamekuwa wamejipanga lakini changamoto mojawapo ni kukabiliana na matukio hayo ambayo mengine ni mapya.

"Jeshi la Polisi wataendelea kukabiliana na matukio ya uhalifu ambayo mengine ni mapya na tutatumia matukio hayo kujifunza ili yasitokee tena," amesema.Hata hivyo Lugola amesema kwamba zipo Sababu nyingi za jumla ambazo zinasababisha kutokea matukio ya watu kutekwa na miongoni mwa sababu ni mambo ya kisiasa,kulipiza kisasi na masuala ya mapenzi.

"Kikubwa tunaomba mtuamini ,tunaendelea kukabiliana na kila aina ya tukio lolote ambalo litatokea tutalifanyia kazi," amesema Waziri Lugola.
Wakati huo huo amesema kuwa thamani ya Watanzania wote ni sawa na inapotokea mmoja wetu amepatwa na tatizo basi Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vitashughulikia kwa uzito sawa.

Amesema kwamba tukio la kutekwa kwa MO linashughulikiwa kama ambavyo yanashughulikiwa matukio mengine na kuomba vyombo vya habari kitenda haki kwa kuacha upendeleo kwa kuandika habari kwa usawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...