Na Tiganya Vincent
MKUU  wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla amewataka wazazi Mkoani Tabora kutowazuia watoto wao kushiriki katika shughuli mbalimbali za elimu ya kujtegemea kama vile ufugaji na utunzaji wa mifugo ya shughuli na kulima mashamba ya shule yao ili ziweze kuwajengea ujuzi utakaowasaidia baadaye.

Alisema elimu ya kujitegemea inamwezesha mwanafunzi hata kabla au baada ya kumaliza elimu yake ya Msingi kuwa na ujuzi wa kufanya shughuli mbalimbali kitalaamu ikiwemo  kuachana kilimo au ufugaji wa kizamani ambacho hakina tija.

Makalla alitoa kauli hiyowilayani Uyui mkoani Tabora wakati wa ziara ya viongozi wa Mkoa wa Katavi  kujifunza juu ya uendeshaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania ambao wanatarajia kuanza kuutekeleza katika eneo lao.

Alisema elimu ya kujitegemea itawasaidia watoto kutoa ujuzi walioupata shuleni na kuupeleka ujuzi huo kwa wazazi wao na hivyo kuwa na uzalishaji wa mifugo na mazao ya kilimo kwa tija.

“Mtoto akielimishwa juu ya upandaji kwa kuzingatia vipimo na mistari tangu shule atasaidia kuambukiza elimu hiyo kwa wazazi wake na hivyo kuwa na uzalishaji wa bidhaa nyingi kwa matumizi yao na viwanda vyetu” alisema.

Makalla alisema wazazi wakiona watoto wao wanafundishwa elimu ya kujitegemea kama vile ufugaji , kilimo cha kisasa, wasione kama ni adhabu bali ni faida kubwa wanayopatiwa watoto wao na jamii kwa ujumla.

Aidha Mkuu huyo wa Katavi na ujumbe wake umefurahishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuinua elimu na kuongeza kipato katika shule mbalimbali mkoani Tabora chini ya Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania.

Alisema kwa kutumia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania Halmashauri kama ile ya Wilaya ya Tabora -Uyui imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi ILolangulu kwa kiasi cha shilingi milioni 35.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla (mwenye miwani) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Uyui mara baada ya kutembelea mradi wa ufugaji kuku  chini ya Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP wakati walipotembelea Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kujifunza.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla (mwenye miwani) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)  Said Ntahondi (kulia) wakiwa kwenye  moja wa madarasa wakati alipoongoza ujumbe kutoka Mkoa wake kuja Tabora kujifunza utekelezaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP.
 Afisa Taaluma Mkoa wa Tabora (RAO) Silvano Sichone akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP kwa ujumbe wa Mkoa wa Katavi  walipofika Mkoani humo kwa ajili ya kujifunza mafanikio yaliyotokana na mpango huo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla miwani) alizungumza na walimu wa Shule ya Msingi Majengo(hawapo katika picha) wakati alipotembelea Mkoa wa Tabora kujifunza jinsi ya utekelezaji wa   Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP. Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...