Na. Vero Ignatus, Arusha

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amelazimika kusitisha ziara kwa masaa mawili na nusu akisubiri kisima katika kijiji cha Levolosi Kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru kinachochimbwa kitoe maji kabla ya kwenda kusaini mkataba.

Aidha Prof. Makame Mbarawa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumrudisha Wizarani mara moja Mhandisi wa Miamba Amir Msangi kwa uzembe wa kutoonekana kwenye eneo la mradi.

Waziri alitoa agizo hilo jana wakati alipotembelea Kijiji cha Levolosi, Kata ya Kimnyaki kujionea zoezi la uchimbaji wa visima vitatu na baada ya hapo alitia saini ya mkataba wa ujenzi wa mtandao mpya wa maji,mitambo ya kutibu maji safi ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA na ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA Kanda ya Kati wenye thamani ya Sh.bilioni 520.

Prof.Mbarawa alisema serikali imeamua kuleta wataalam wake toka Wizarani ili wasimamie na kujifunza Teknolojia mpya ya uchimbaji visima vikubwa kwa ajili ya kuweza kufundiaha wenzao utaalam huo hapo baadaye.

"Lakini cha kushangaza nimepata taarifa huyu Amir Msangi haonekani eneo la kazi na hivyo namwagiza mtaalam mwenzake Fatuma Mambo kumtaarifu Katibu Mkuu ili arudishwe Wizarani huyu na hapa aletwe mwingine atakayepata ujuzi huu,"alisema.Amesisitiza kuwa lengo kubwa la serikali ni kuwaleta wataalam hao ili kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa inakuwa na ubora uliokusudiwa.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wananchi kupata maji kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.Aidha alisema miradi hiyo inatekelezwa na AUWSA kwa ufadhili wa serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Mhe Mbarawa akiongozwa na wataalamu wa kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd kuangalia mwamba unaotoa maji ardhini kwa kutumia camera maalumu. Picha na Vero Ignatus. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Mbarawa akikagua urefu wa kisima katika kijiji cha Levolosi kata ya Kimnyaki akiwa ameambatana na wahandisi toka wizara ya maji na mamlaka ya maji safi na usafishaji jijinla Arusha AUWSA. Picha na Vero Ignatus


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...