Na Mwandishi Wetu, London 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mawaziri wake Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Wazirri wa Katika na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wameweza kuhutubia mkutano mkubwa na wa Kimataifa juu ya upigaji vita biashara haramu ya nyara, uliokuwa wa siku mbili Oktoba 11 na 12, 2018, Jijini London, Uingereza.

Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi wamuwakilisha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo wa Kimataifa na kuandaliwa na Serikali ya Uingereza chini ya Uenyekiti wa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William.

Mwaka huu mkutano huo ni wa Nne wa Ngazi ya juu kuhusu Biashara haramu ya nyara ambao huku ukiwakutanisha viongozi wakuu wa nchi, mawaziri na wataalam kutoka zaidi ya nchi 60 Duniani pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, wasomi na wafanyabiashara.

Mkutano huo una lengo la kuimarisha jitahada zinazofanywa na Serikali mbalimbali duniani katika kupambana na kuzuia biashara haramu ya nyara.Mawaziri hao wa Tanzania kwa nyakati tofauti wameweza kusoma hotuba zao zenye malengo ya na jitihada za Serikali ya Tanzania katika uhifadhi wa Maliasili na kupambana na biashara haramu ya nyara hususani katika hifadhi zake za taifa na maeneo yote ya mapori ya hakiba sambamba na shoroba zilizopo.

Imeelezwa kuwa, Tanzania ni moja ya nchi ambayo imetenga asilimia 32.5% ya eneo lake kwa ajili ya uhifadhi na inasifika kwa uwingi wa bayoanuai. Jitiada za kuzuia ujangili zimepelekea kupungua kwa ujangili kwa asilimia 50 na hii imejidhihirisha kwa kuongezeka kwa Tembo kutoka 43330 mwaka 2014 hadi kufikia tembo 59830 mwaka 2015. Kwa zaidi ya Asilimia 60 

Wakati akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Mkutano huo Prince William wa Uingereza alisifu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika uhifadhi na upambanaji wa Biashara haramu ya nyara.Prince William alipongeza jitihada alizozishuhudia wakati wa ziara yake nchini Tanzania zikiwemo kutoka Elimu ya uhifadhi kwa wanafunzi pamoja na vyuo vizuri vya Elimu ya uhifadhi kikiwemo Chuo cha Elimu ya Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka.

Madhumuni ya mkutano huo ni kujenga ushirikiano baina ya nchi, taasisi binafsi na za kiserikali, NGOs na Wanataaluma, pia unalengo la kubadilishana uzoefu na mbinu za kupunguza mahitaji ya soko la nyara kwa nia ya kulifunga soko hilo duniani.
Waziri Dkt. Kigwangalla na Waziri Prof. Kabudi wakiwa katika mkutano huo. 
Waziri Dkt. Kigwangalla na Waziri Prof. Kabudi wakiwa wakibadilishana mawazo na wadau wa masuala ya wanyama kwenye muda wa mijadala wakati wa mkutano huo 
Waziri Dkt. Kigwangalla akizungumza katika mkutano 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...