Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam(DART) Mhandisi Ronald Lwakatare amepewa onyo kwa kile kinachoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Onyo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Suleiman Jafo ambapo pia amemtaka Mhandisi Lwakatare kujieleza kwanini ameshidwa kumsimamia mtoa huduma Udart.

Waziri Jafo mbali ya kutoa onyo hilo ametoa maagizo kwa Naibu Waziri wake Joseph Kakunda kufanya kikao ambacho kitamjumuisha Mtendaji mkuu wa Dart pamoja na mtoa huduma Udart ili kubaini changamoto zilizopo ambazo zinasababisha usafiri huo kuonekana kero kwa wananchi.

Amefafanua usafiri wa mabasi ya mwendo kasi ni usafiri uliokuwa wa nema kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wengi wao walikuwa wanatumia zaidi ya saa tatu kutoka Posta hadi Kimara.

"Leo hii kupitia usafiri huu wanatumia takribani dakika 40 hadi 45, hivyo hatuwezi kuacha huduma ziendele kudorola kwa kiasi hichi.Lazima ufumbuzi upatikane ili wananchi wafurahie huduma za usafiri huo,"amesisitiza Jafo.

Wakati huo huo Waziri Jafo amemtaka Katibu Mkuu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhandisi Mussa Iyombe kufanya uchunguzi katika ofisi ya Dart ili kuona kama wapo watendaji ambao wanakwamisha huduma hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...