Na Baltazar Mashaka, Mwanza 
HALMASHAURI ya Manipaa ya Ilemela imeagizwa kukusanya na kusimamia mapato ili kusukuma maendeleo kwa maslahi ya wananchi.

Agizo hilo lilitolewa na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wakati akikagua miradi ya ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri hiyo,barabara na hospitali ya Wilaya ya Ilemela.

Alisema kuwa halmashauri hiyo haikufanya vizuri kwenye mapato baada ya kukusanya sh.bilioni 4.6 kati ya bilioni 5.7 ya makisio ya bajeti na hivyo kusababisha ishike nafasi ya mwisho ambapo awali ilikisia kukusanya bilioni 11.7.

Jafo alisema kwenye amebini halmshauri nyingi zimegubikwa na mianya ya upotevu wa fedha za mapato kwa kutumia mashine za Possy ambapo fedha zinazokusanywa kwenye mfumo ni tofauti na baadhi ya watu wanakimbia na fedha huku wengine wakibaki nazo.

 “Agenda ya serikali ni mapato hivyo watumishi badilikeni kiutendaji, maana mapato hayo yanatakiwa kusukuma maendeleo ya wananchi na halmashauri haziwezi kujiendesha bila mapato .Ilemela ni tajiri lakini imefanya vibaya na kuharibu sifa ya Mkuu wa Mkoa, Wilaya na Mkuerugenzi sababu ya uzembe wa watendaji, ni aibu na tafakarini mbadilike,”alisema.

Aliwaagiza Meya  Manispaa hiyo Renatus Mulunga na Mkurugenzi  John Wanga pamoja na kamati ya fedha kusimamia mapato yote kwa umakini kwa sababu wamepewa dhamana hiyo kwa ajili ya Watanzania  wanyonge.
 Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua miradi ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
  Mhandisi Charles Mathias wa kampuni ya Ushauri ya Nimeta Consultancy akimwelekeza jambo Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wakati akikagua jengo la utawala la Manispaa ya Ilemela.kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
 Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiangalia ramani ya mradi wa ujenzi wa jengo la kituo cha afya Buzuruga alipoafanya ziara katika Wilaya ya Ilemela.
 Selemani Jafo ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akizungumza na baadhi ya wananchi na watumishi wa kituo cha afya Buzuruga kabla ya kukagua uboreshaji wa majengo ya kituo hicho.
Mhandisi Peter Marmo anayetekeleza mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya majengo ya kituo cha Afya buzuruga katika Manispaa ya Ilemela akimweleza jambo Waziri wa Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi inayotekelezwa chini ya wizara hiyo. Picha Zote na Baltazar Mashaka.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...