IMEELEZWA kuwa kukamilika mapema kwa barabara za lami na madaraja ya kisasa katika mkoa wa Ruvuma kutauunganisha kirahisi na mikoa ya nyanda za juu kusini na nchi za jirani na hivyo kuhuisha uchumi wa wakazi wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amesema hayo alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 60 na kumtaka mkandarasi china Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO), anayejenga barabara hiyo kuikamilisha kwa wakati.
Amesema fursa za kilimo, uvuvi, usafirishaji na uchukuzi wa mazao na makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma zinahitaji barabara za lami na zenye uwezo wa kupitika wakati wote na kwa urahisi hivyo kukamilika kwa barabara za lami kwa wakati kutaleta ukombozi kwa wananchi wa mkoa huo.
“Viwanda vingi sasa vinatumia makaa ya mawe tena kwa kiwango kikubwa hivyo tunahakikisha usafiri katika mkoa huu unakuwa wa uhakika ili kuufungua na kuunganisha na mikoa mingine kwa njia fupi  na  hivyo kuongeza biashara ya ndani kuvutia biashara na nchi za jirani”, amesema Mhandisi Kamwelwe.
Amesisitiza kuwa  Serikali imejipanga kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara za Ikuyufusi –Mkenda,  Kitae-Lituhi KM 84.5, Lituhi –Mbamba Bay KM 112.5 na kukamilisha kwa wakati daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Ruvuma na Njombe kupitia Ludewa ili kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi mkoani Ruvuma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), mara baada ya kukagua kivuko cha Mv. Ruhuhu kinachotoa huduma kwa wakazi wa Wilaya za Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma na Ludewa mkoani Njombe.
 Muonekano wa makaa ya mawe katika kijiji cha Ikuyufusi, Serikali imeamua kujenga barabara ya lami kati ya Ikuyufusi na Mkenda ili kuwezesha shughuli za uchukuzi wa rasilimali hiyo mkoani Ruvuma kutekelezeka kikamilifu. 
 Muonekano wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 60 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Ruvuma.
Muonekano wa mtambo wa kusaga kokoto kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 66 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Ruvuma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...