*Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya maafisa elimu na walimu kutojihusisha na vitendo vya wizi wa mitihani vinavyofanywa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kwa sababu vinawadharirisha.
“Kama kweli umemuandaa mtoto huna sababu ya kuiba mitihani na mtoto hawezi kufikiria kuiba mitihani kwa sababu yuko nje ya mfumo. Walimu heshimuni maadili ya kazi ya ualimu.”
Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumanne, Oktoba 9, 2018) baada ya kukabidhiwa vyumba vya madarasa vya shule za msingi Nyakato na Kashozi, wilayani Bukoba.
Vyumba hivyo vilivyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japan baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwaka 2016.
Waziri Mkuu amesema tathmini ya elimu katika shule za msingi na sekondari hufanyika kwa kufanya mitihani, dosari ya udanganyifu wa mitihani iliyojitokeza katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu isijirudie tena.
Wiki iliyopitaBaraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilifuta matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa shule za msingi zote za Halmashauri ya Chemba na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuvujisha mitihani.
Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imechukua hatua kali kwa watu wote walioshiriki katika kitendo hicho kwa sababu kinadumaza uelewa na ufikiri kwa wanafunzi, hivyo kuwaandaa watoto kuwa wategemezi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kupokea
madarasa mapya yaliyojengwa kwa Masada wa serikali ya Japan katika Shule
ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 8, 2018. Kulia kwake ni
Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Katsutoshi Takeda. Majengo ya
shule hiyo yaliharibiwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa
Kagera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua
madaras mapya yaliyojengwa kwa Masada wa serikali ya Japan katika Shule
ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 8, 2018. Kushoto ni
Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Katsutoshi Takeda (kushoto).
Majengo ya shule hiyo yaliharibiwa na tetemeko la ardhi lililoukumba
mkoa wa Kagera.(
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Bw.
Katsutoshi Takeda wakiwa kwenye moja ya madarasa yaliyojengwa kwa
ufadhili wa serikali ya Japan katika shule ya msingi ya Nyakato wilayani
Bukoba ambayo iliharibiwa na tetemeko la ardhi. Madarasa hayo
yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Oktoba 9, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea funguo kutoka kwa Mwakilishi wa Balozi
wa Japan Nchini, Katsutoshi Takeda ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa
madarasa yaliyojengwa na serikali ya Japan katika Shule ya Msingi ya
Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 9, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanafunzi baada ya kupokea madarasa
yaliyojengwa kwa masada wa serikali ya Japan katika shule ya msingi ya
Nyakato wilayani Bukoba ambayo iliharibiwa na tetemeko la ardhi la
Kagera. Madarasa hayo yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mwakilishi wa
Balozi wa Japan nchini, Bw. Katsutoshi Takeda, Oktoba 9, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...